Ash-Shams

الشمس

The Sun15 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا﴿١

1Ninaapa kwa jua na mwangaza wake!

وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا﴿٢

2Na kwa mwezi unapolifuatia!

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا﴿٣

3Na kwa mchana unapolidhihirisha!

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا﴿٤

4Na kwa usiku unapolifunika!

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا﴿٥

5Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga!

وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا﴿٦

6Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza!

وَنَفۡسٖ وَمَا سَوَّىٰهَا﴿٧

7Na kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza!

فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا﴿٨

8Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا﴿٩

9Hakika amefanikiwa aliyeitakasa.

وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا﴿١٠

10Na hakika amehasiri aliyeiviza.

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ﴿١١

11Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotovu wao.

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا﴿١٢

12Aliposimama mwovu wao mkubwa.

فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا﴿١٣

13Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipowaambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا﴿١٤

14Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.

وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا﴿١٥

15Wala Yeye haogopi matokeo yake.

RELATED SURAHS