An-Nazi'at

النازعات

Those Who Drag Forth46 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا﴿١

1Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu.

وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا﴿٢

2Na kwa wanaotoa kwa upole.

وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا﴿٣

3Na wanaoogelea sawasawa.

فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا﴿٤

4Wakishindana mbio kweli kweli.

فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا﴿٥

5Wakidabiri mambo.

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ﴿٦

6Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka.

تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ﴿٧

7Kifuate cha kufuatia.

قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ﴿٨

8Siku hiyo nyoyo zitapigapiga.

أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ﴿٩

9Macho yatainama chini.

يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ﴿١٠

10Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?

أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ﴿١١

11Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa?

قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ﴿١٢

12Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara!

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ﴿١٣

13Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu.

فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ﴿١٤

14Mara watakuwa kwenye Uwanda wa mkutano!

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ﴿١٥

15Je! Imekufikia hadithi ya Musa?

إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى﴿١٦

16Mola wake Mlezi alipomwita katika bonde takatifu la Tuwaa, akamwambia:

ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ﴿١٧

17Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.

فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ﴿١٨

18Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?

وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ﴿١٩

19Nami nitakuongoza ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.

فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ﴿٢٠

20Basi alimwonyesha Ishara kubwa.

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ﴿٢١

21Lakini alikadhibisha na akaasi.

ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ﴿٢٢

22Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ﴿٢٣

23Akakusanya watu akanadi.

فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ﴿٢٤

24Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.

فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ﴿٢٥

25Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ﴿٢٦

26Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa Mwenyezi Mungu.

ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا﴿٢٧

27Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliyeijenga!

رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا﴿٢٨

28Akainua paa lake, na akaitengeneza vizuri.

وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا﴿٢٩

29Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.

وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ﴿٣٠

30Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.

أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا﴿٣١

31Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake.

وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا﴿٣٢

32Na milima akaisimamisha imara.

مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ﴿٣٣

33Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ﴿٣٤

34Basi itakapofika hiyo Balaa kubwa,

يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ﴿٣٥

35Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya,

وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ﴿٣٦

36Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ﴿٣٧

37Basi ama yule aliyezidi ujeuri,

وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا﴿٣٨

38Na akakhiari maisha ya dunia,

فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ﴿٣٩

39Kwa hakika Jahannamu ndiyo makazi yake!

وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ﴿٤٠

40Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,

فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ﴿٤١

41Basi huyo, Bustani ya mbinguni itakuwa ndiyo makazi yake!

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا﴿٤٢

42Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ﴿٤٣

43Una nini wewe hata uitaje?

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ﴿٤٤

44Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.

إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا﴿٤٥

45Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu.

كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا﴿٤٦

46Ni kama kwamba wao siku watakapoiona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.

RELATED SURAHS