'Abasa

عبس

He Frowned42 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ﴿١

1Alikunja kipaji na akageuka mbali.

أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ﴿٢

2Kwa sababu alimjia kipofu!

وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ﴿٣

3Na nini kitakachokujulisha pengine yeye atatakasika?

أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ﴿٤

4Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?

أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ﴿٥

5Ama ajionaye hana haja,

فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ﴿٦

6Wewe ndiyo unamshughulikia?

وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ﴿٧

7Na si juu yako kama hakutakasika.

وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ﴿٨

8Ama anayekujia kwa juhudi.

وَهُوَ يَخۡشَىٰ﴿٩

9Naye anaogopa,

فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ﴿١٠

10Ndiyo wewe unampuuza?

كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ﴿١١

11Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ﴿١٢

12Basi anayependa akumbuke.

فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ﴿١٣

13Yamo katika kurasa zilizoheshimiwa.

مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ﴿١٤

14Zilizoinuliwa, zilizotakaswa.

بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ﴿١٥

15Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,

كِرَامِۭ بَرَرَةٖ﴿١٦

16Watukufu, wema.

قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ﴿١٧

17Ameangamia mwanadamu! Nini kinachomkufurisha?

مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ﴿١٨

18Kwa kitu gani amemuumba?

مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ﴿١٩

19Kwa tone la manii, amemuumba na akamkadiria.

ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ﴿٢٠

20Kisha akamsahilishia njia.

ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ﴿٢١

21Kisha akamfisha, akamtia kaburini.

ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ﴿٢٢

22Kisha apendapo atamfufua.

كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ﴿٢٣

23La! Hajamaliza aliyomuamuru.

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ﴿٢٤

24Hebu mtu na atazame chakula chake.

أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا﴿٢٥

25Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu.

ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا﴿٢٦

26Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu.

فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا﴿٢٧

27Kisha tukaotesha humo nafaka.

وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا﴿٢٨

28Na zabibu, na mimea ya majani.

وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا﴿٢٩

29Na mizaituni, na mitende.

وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا﴿٣٠

30Na bustani zenye miti iliyosongana barabara.

وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا﴿٣١

31Na matunda, na malisho ya wanyama.

مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ﴿٣٢

32Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ﴿٣٣

33Basi utakapokuja Ukelele.

يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ﴿٣٤

34Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye.

وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ﴿٣٥

35Na mamaye na babaye.

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ﴿٣٦

36Na mkewe na wanawe.

لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ﴿٣٧

37Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ﴿٣٨

38Siku hiyo ziko nyuso zitakazonawiri.

ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ﴿٣٩

39Zitacheka, zitachangamka.

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ﴿٤٠

40Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi.

تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ﴿٤١

41Giza totoro litazifunika.

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ﴿٤٢

42Hao ndio makafiri watenda maovu.

RELATED SURAHS