الرحمن
The Most Merciful • 78 ayahs • Medinan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Arrah'man (Mwingi wa Rehema).
2Amefundisha Qur-ani.
3Amemuumba mwanadamu.
4Akamfundisha kubaini.
5Jua na mwezi huenda kwa hesabu.
6Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
7Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani.
8Ili msidhulumu katika mizani.
9Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
10Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
11Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
12Na nafaka zenye makapi, na rehani.
13Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha.
14Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.
15Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
16Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha
17Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
18Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
19Anaziendesha bahari mbili zikutane.
20Baina yake kipo kizuizi, zisiingiliane.
21Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
22Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
23Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
24Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyoundwa kama milima.
25Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
26Kila kilichoko juu yake kitatoweka.
27Na utabakia uso wa Mola wako Mlezi, wenye utukufu na ukarimu.
28Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
29Vinamwomba Yeye vilivyo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
30Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
31Tutakufanyieni hesabu enyi makundi mawili.
32Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
33Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa mamlaka.
34Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
35Mtatumiwa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
36Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
37Itakapopasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
38Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
39Basi Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
40Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
41Watajuulikana wahalifu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
42Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
43Hii ndiyo Jahannamu ambayo wahalifu walikuwa wakiikanusha.
44Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayochemka.
45Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
46Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
47Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
48Bustani zenye matawi yaliyotanda.
49Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
50Ndani yake zimo chemichemi mbili zinazopita.
51Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
52Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
53Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
54Wawe wameegemea matandiko yenye bitana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
55Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
56Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
57Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
58Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
59Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha.
60Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
61Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
62Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyingine mbili.
63Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
64Za kijani kibivu.
65Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
66Na chemichemi mbili zinazofurika.
67Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
68Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
69Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
70Humo wamo wanawake wema wazuri.
71Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
72Wanawake wazuri wanaotawishwa katika mahema.
73Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
74Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
75Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
76Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
77Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
78Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.