An-Nahl

النحل

The Bee128 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ﴿١

1Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiiharakishe. Ametakasika na ametukuka mbali na hayo wanayomshirikisha nayo.

يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ﴿٢

2Huwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi, basi nicheni Mimi.

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ﴿٣

3Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ﴿٤

4Amemuumba mtu kwa tone la manii. Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri.

وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ﴿٥

5Na aliwaumba wanyama. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.

وَلَكُمۡ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسۡرَحُونَ﴿٦

6Na katika hao mnapata furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi.

وَتَحۡمِلُ أَثۡقَالَكُمۡ إِلَىٰ بَلَدٖ لَّمۡ تَكُونُواْ بَٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلۡأَنفُسِۚ إِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ﴿٧

7Nao hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.

وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡكَبُوهَا وَزِينَةٗۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ﴿٨

8Na farasi, nyumbu, na punda ili muwapande, na wawe ni pambo. Na anaumba msivyovijua.

وَعَلَى ٱللَّهِ قَصۡدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنۡهَا جَآئِرٞۚ وَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ﴿٩

9Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu. Na angelipenda, angeliwaongoa nyote.

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗۖ لَّكُم مِّنۡهُ شَرَابٞ وَمِنۡهُ شَجَرٞ فِيهِ تُسِيمُونَ﴿١٠

10Yeye ndiye anayewateremshia maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia.

يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرۡعَ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلۡأَعۡنَٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ﴿١١

11Kwa hayo Yeye anawaoteshea mimea, na mizaituni, na mitende, na mizabibu, na kila aina ya matunda. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaotafakari.

وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ﴿١٢

12Na amewatiishia usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili.

وَمَا ذَرَأَ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣

13Na vile alivyowaenezea katika ardhi vya rangi mbalimbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaokumbuka.

وَهُوَ ٱلَّذِي سَخَّرَ ٱلۡبَحۡرَ لِتَأۡكُلُواْ مِنۡهُ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُواْ مِنۡهُ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ﴿١٤

14Yeye ndiye aliyeitiisha bahari, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa. Na utaona merikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.

وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَأَنۡهَٰرٗا وَسُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ﴿١٥

15Na akaweka katika ardhi milima madhubuti ili ardhi isiyumbeyumbe nanyi. Na mito, na njia mbalimbali ili mpate kuongoka.

وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ﴿١٦

16Na alama nyinginezo. Na kwa nyota wao wanajiongoza.

أَفَمَن يَخۡلُقُ كَمَن لَّا يَخۡلُقُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٧

17Ati yule anayeumba ni kama asiyeumba? Basi hebu hamkumbuki?

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ﴿١٨

18Na mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira mno, Mwingi wa kurehemu.

وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ﴿١٩

19Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadharani.

وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ﴿٢٠

20Na wale wanaowaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa.

أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ﴿٢١

21Ni wafu, si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini.

إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ﴿٢٢

22Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanatakabari.

لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ﴿٢٣

23Hakuna shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua yale wanayoyaficha na wanayoyaweka hadharani. Hakika, Yeye hawapendi wanaotakabari.

وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡ قَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿٢٤

24Na wanapoambiwa, "Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?" Husema: Hadithi za kubuni za wa mwanzo!

لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ﴿٢٥

25Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Angalia, ni mabaya mno hayo wanayoyabeba!

قَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنۡيَٰنَهُم مِّنَ ٱلۡقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّقۡفُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَأَتَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ﴿٢٦

26Walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, naye Mwenyezi Mungu akayajia majengo yao kutokea kwenye misingi, kwa hivyo dari zake zikaporomoka juu yao, na adhabu ikawajia kutokea wasipohisi.

ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُخۡزِيهِمۡ وَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تُشَٰٓقُّونَ فِيهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ إِنَّ ٱلۡخِزۡيَ ٱلۡيَوۡمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ﴿٢٧

27Kisha Siku ya Kiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkipinga (Manabii)? Watasema wale waliopewa elimu: Hakika leo ndiyo hizaya na ubaya vitawashukia makafiri.

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡۖ فَأَلۡقَوُاْ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعۡمَلُ مِن سُوٓءِۭۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ﴿٢٨

28Wale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu nafsi zao! Basi wanasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya ubaya wowote. (Wataambiwa). Hasha! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda.

فَٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ فَلَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩

29Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni mabaya mno makazi ya wafanyao kiburi!

۞ وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡۚ قَالُواْ خَيۡرٗاۗ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۚ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞۚ وَلَنِعۡمَ دَارُ ٱلۡمُتَّقِينَ﴿٣٠

30Na wataambiwa wale waliomcha Mungu: Mola wenu Mlezi aliteremsha nini? Watasema: "Heri." Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na ni njema mno nyumba hiyo ya wacha Mungu.

جَنَّٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ لَهُمۡ فِيهَا مَا يَشَآءُونَۚ كَذَٰلِكَ يَجۡزِي ٱللَّهُ ٱلۡمُتَّقِينَ﴿٣١

31Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kwa chini yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha.

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ﴿٣٢

32Wale ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri, wanawaambia: Salama iwe juu yenu! Ingieni Bustanini kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ أَمۡرُ رَبِّكَۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ﴿٣٣

33Wanangojea jingine hawa isipokuwa Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi? Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe.

فَأَصَابَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُواْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ﴿٣٤

34Basi yakawafikia mabaya ya yale waliyoyatenda, na yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai yakawazingira.

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ﴿٣٥

35Na washirikina walisema: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharamisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo, walifanya wale waliokuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi?

وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ﴿٣٦

36Na hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Twaghut. Basi kati yao wapo aliowaongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao uliwathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wale wanaokadhibisha.

إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ﴿٣٧

37Hata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao, basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru.

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ﴿٣٨

38Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua aliyekufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini wengi wa watu hawajui.

لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ﴿٣٩

39Ili awabainishie yale waliyohitilafiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.

إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ﴿٤٠

40Hakika, kauli yetu kwa kitu tunapokitaka kiwe, ni kukiambia tu: "Kuwa!" Basi kinakuwa.

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ﴿٤١

41Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya shaka tutawaweka katika maskani mazuri katika dunia; na hakika ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; lau wangekuwa wanajua!

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ﴿٤٢

42Wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ﴿٤٣

43Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume tuliowapa ufunuo (wahyi). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.

بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤

44Kwa Ishara wazi na Vitabu. Na tumekuteremshia ukumbusho huu ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, ili wapate kutafakari.

أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخۡسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ يَأۡتِيَهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ﴿٤٥

45Je wana amani wale wanaopanga njama mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafikia adhabu kutoka wasipohisi?

أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ فِي تَقَلُّبِهِمۡ فَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ﴿٤٦

46Au hatawashika katika harakati zao, na wala hawatamshinda?

أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ عَلَىٰ تَخَوُّفٖ فَإِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٌ﴿٤٧

47Au hatawashika huku wana hofu? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu.

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ يَتَفَيَّؤُاْ ظِلَٰلُهُۥ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدٗا لِّلَّهِ وَهُمۡ دَٰخِرُونَ﴿٤٨

48Je, hawavioni vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu, vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, vikimsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea?

وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ﴿٤٩

49Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama mpaka Malaika na wala havitakabari.

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوۡقِهِمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ۩﴿٥٠

50Vinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa.

۞ وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓاْ إِلَٰهَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَإِيَّٰيَ فَٱرۡهَبُونِ﴿٥١

51Na Mwenyezi Mungu amesema: Msijifanyie miungu wawili! Hakika Yeye ndiye Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni sana Mimi tu!

وَلَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًاۚ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ﴿٥٢

52Na ni vyake Yeye vilivyo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je, mnamcha mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu?

وَمَا بِكُم مِّن نِّعۡمَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيۡهِ تَجۡـَٔرُونَ﴿٥٣

53Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakiwagusa madhara, mnamyayatikia Yeye.

ثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنكُم بِرَبِّهِمۡ يُشۡرِكُونَ﴿٥٤

54Na anapowaondoshea madhara hayo, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi.

لِيَكۡفُرُواْ بِمَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡۚ فَتَمَتَّعُواْ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ﴿٥٥

55Wakizikataa neema tulizowapa. Basi stareheni. Mtakujajua!

وَيَجۡعَلُونَ لِمَا لَا يَعۡلَمُونَ نَصِيبٗا مِّمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡۗ تَٱللَّهِ لَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَفۡتَرُونَ﴿٥٦

56Na hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu katika vile tunavyowaruzuku. Tallahi! Bila ya shaka mtaulizwa kwa hayo mliyokuwa mnayazua!

وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ ٱلۡبَنَٰتِ سُبۡحَٰنَهُۥ وَلَهُم مَّا يَشۡتَهُونَ﴿٥٧

57Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu mabinti, Subhanahu (ametakasika)! Na wao wenyewe, ati ndiyo wana hayo wanayoyatamani!

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِٱلۡأُنثَىٰ ظَلَّ وَجۡهُهُۥ مُسۡوَدّٗا وَهُوَ كَظِيمٞ﴿٥٨

58Na mmoja wao akibashiriwa msichana, uso wake unasalia umesawijika na anakuwa na huzuni mno.

يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓۚ أَيُمۡسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمۡ يَدُسُّهُۥ فِي ٱلتُّرَابِۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ﴿٥٩

59Anajificha asionekane na watu kwa sababu ya ubaya wa yule aliyebashiriwa! Je, akae naye pamoja na fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama, ni ubaya mno wanavyohukumu!

لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوۡءِۖ وَلِلَّهِ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ﴿٦٠

60Wale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلۡمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيۡهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ﴿٦١

61Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha juu yake hata mnyama mmoja. Lakini anawaahirisha mpaka muda uliowekwa. Na unapofika muda wao, hawatakawia hata saa moja wala hawatatangulia.

وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكۡرَهُونَۚ وَتَصِفُ أَلۡسِنَتُهُمُ ٱلۡكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفۡرَطُونَ﴿٦٢

62Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyovichukia wao, na ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mazuri zaidi. Hakuna shaka kwamba hakika wana Moto, na kwamba kwa yakini wataachwa humo.

تَٱللَّهِ لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ﴿٦٣

63Tallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini Shetani akawapambia matendo yao. Kwa hivyo leo, yeye ndiye kipenzi chao msaidizi, nao wana adhabu chungu.

وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ﴿٦٤

64Na hatukukuteremshia Kitabu hiki isipokuwa ili uwabainishie yale ambayo wanahitilafiana ndani yake, na kiwe uwongofu na rehema kwa kaumu wanaoamini.

وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ﴿٦٥

65Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika, katika hayo imo Ishara kwa kaumu wanaosikia.

وَإِنَّ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَنۡعَٰمِ لَعِبۡرَةٗۖ نُّسۡقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيۡنِ فَرۡثٖ وَدَمٖ لَّبَنًا خَالِصٗا سَآئِغٗا لِّلشَّٰرِبِينَ﴿٦٦

66Na hakika katika wanyama wa kufugwa[1], mna mazingatio. Tunawanywesha katika vile vilivyomo matumboni mwao - baina ya mavi na damu - maziwa safi, mazuri kwa wanywao.

وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلۡأَعۡنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنۡهُ سَكَرٗا وَرِزۡقًا حَسَنًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ﴿٦٧

67Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza vileo na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili.

وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِي مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ﴿٦٨

68Na Mola wako Mlezi alimfunulia nyuki kwamba: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika vile wanavyojenga watu.

ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسۡلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلٗاۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٞ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٞ لِّلنَّاسِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩

69Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizofanywa nyepesi kuzipita. Na kwenye matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponya kwa watu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa kaumu wanaotafakari.

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ﴿٧٠

70Na Mwenyezi Mungu aliwaumba; kisha atawafisha. Na miongoni mwenu wapo wanaorudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa hajui kitu baada ya kuwa alikuwa anajua. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi, Muweza.

وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعۡضَكُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلرِّزۡقِۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُواْ بِرَآدِّي رِزۡقِهِمۡ عَلَىٰ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَهُمۡ فِيهِ سَوَآءٌۚ أَفَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ﴿٧١

71Na Mwenyezi Mungu amewaboresha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walioboreshwa hawarudishi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةٗ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِۚ أَفَبِٱلۡبَٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَتِ ٱللَّهِ هُمۡ يَكۡفُرُونَ﴿٧٢

72Na Mwenyezi Mungu amewaumbia wake kutokana na nyinyi wenyewe, na akawafanyia kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akawaruzuku vitu vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu?

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ رِزۡقٗا مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ﴿٧٣

73Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasiowamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu.

فَلَا تَضۡرِبُواْ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡثَالَۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ﴿٧٤

74Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

۞ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبۡدٗا مَّمۡلُوكٗا لَّا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَمَن رَّزَقۡنَٰهُ مِنَّا رِزۡقًا حَسَنٗا فَهُوَ يُنفِقُ مِنۡهُ سِرّٗا وَجَهۡرًاۖ هَلۡ يَسۡتَوُۥنَۚ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ﴿٧٥

75Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliyemruzuku riziki njema inayotoka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi (sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu)! Lakini wengi wao hawajui.

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا رَّجُلَيۡنِ أَحَدُهُمَآ أَبۡكَمُ لَا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوۡلَىٰهُ أَيۡنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأۡتِ بِخَيۡرٍ هَلۡ يَسۡتَوِي هُوَ وَمَن يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ﴿٧٦

76Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanaume wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa mlezi wake. Popote anapomuelekeza, haleti heri yoyote. Je, huyo anaweza kuwa sawa na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَآ أَمۡرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمۡحِ ٱلۡبَصَرِ أَوۡ هُوَ أَقۡرَبُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ﴿٧٧

77Na siri zote za mbinguni na ardhini ni za Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa jambo la Saa (ya Kiyama) isipokuwa kama kupepesa kwa jicho, au chini zaidi ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

وَٱللَّهُ أَخۡرَجَكُم مِّنۢ بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ﴿٧٨

78Na Mwenyezi Mungu aliwatoa matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu, na akawajaalia kusikia na kuona na ufahamu wa nyoyo ili mpate kushukuru.

أَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ مُسَخَّرَٰتٖ فِي جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ﴿٧٩

79Je, hawawaoni ndege walivyotiishwa katika anga la mbingu? Hakuna mwenye kuwashikilia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa kaumu wanaoamini.

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ﴿٨٠

80Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amewajaalia kutokana na ngozi za wanyama, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufu zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda.

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡجِبَالِ أَكۡنَٰنٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلۡحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأۡسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡلِمُونَ﴿٨١

81Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anavyowatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake.

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ﴿٨٢

82Kwa hivyo, wakikengeuka, basi lililo juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu.

يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ﴿٨٣

83Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ﴿٨٤

84Na siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma, kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi.

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلۡعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ﴿٨٥

85Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, hawatapunguziwa adhabu hiyo, wala hawatapewa muhula.

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ شُرَكَآءَهُمۡ قَالُواْ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدۡعُواْ مِن دُونِكَۖ فَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلَ إِنَّكُمۡ لَكَٰذِبُونَ﴿٨٦

86Na wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako." Lakini hao watawatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo!

وَأَلۡقَوۡاْ إِلَى ٱللَّهِ يَوۡمَئِذٍ ٱلسَّلَمَۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ﴿٨٧

87Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu, na yatapotea yale waliyokuwa wakiyazua.

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدۡنَٰهُمۡ عَذَابٗا فَوۡقَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يُفۡسِدُونَ﴿٨٨

88Wale waliokufuru na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu, kwa walivyokuwa wakifanya uharibifu.

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ﴿٨٩

89Na (waonye) siku tutakapomtoa shahidi katika kila umma kutokana na wao wenyewe, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

۞ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠

90Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na dhuluma. Anawaaidhi ili mpate kukumbuka.

وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ﴿٩١

91Na timizeni agano la Mwenyezi Mungu mnapoagana, wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara, ilhali mmekwishamfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo.

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِي نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثٗا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ﴿٩٢

92Wala msiwe kama mwanamke yule aliyeufumua uzi wake baada ya kwishausokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine? Hakika Mwenyezi Mungu anawajaribu kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Kiyama yale mliyokuwa mkihitilafiana ndani yake.

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ﴿٩٣

93Na Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeliwafanya kuwa umma mmoja. Lakini anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ فَتَزِلَّ قَدَمُۢ بَعۡدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُواْ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَكُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ﴿٩٤

94Wala msifanye viapo vyenu kuwa njia ya kudanganyana baina yenu, mguu ukajateleza baada ya kuwa thabiti, na mkaonja mabaya kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa.

وَلَا تَشۡتَرُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ﴿٩٥

95Wala msinunue kwa agano la Mwenyezi Mungu thamani ndogo. Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua.

مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ﴿٩٦

96Mlivyo navyo vitakwisha, na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ﴿٩٧

97Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, hakika tutamhuisha uhai mwema, na hakika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ﴿٩٨

98Na unaposoma Qur-ani, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na Shetani aliyelaaniwa.

إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ﴿٩٩

99Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

إِنَّمَا سُلۡطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوۡنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشۡرِكُونَ﴿١٠٠

100Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, na wale wanaofanya ushirika naye.

وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ﴿١٠١

101Na tunapobadilisha Ishara pahala pa Ishara, na Mwenyezi Mungu anayajua anayoyateremsha, wanasema: "Wewe si chochote ila ni mzushi tu", lakini wengi wao hawajui tu.

قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ﴿١٠٢

102Sema: Ameiteremsha Roho Mtakatifu kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa haki, ili iwaimarishe wale walioamini, na kuwa ni uongofu, na bishara kwa Waislamu.

وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّهُمۡ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُۥ بَشَرٞۗ لِّسَانُ ٱلَّذِي يُلۡحِدُونَ إِلَيۡهِ أَعۡجَمِيّٞ وَهَٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيّٞ مُّبِينٌ﴿١٠٣

103Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: "Hakika yuko mtu anayemfundisha." Lugha ya huyo wanayemuelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu iliyo bainifu.

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَا يَهۡدِيهِمُ ٱللَّهُ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٠٤

104Hakika wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao wana adhabu chungu.

إِنَّمَا يَفۡتَرِي ٱلۡكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ﴿١٠٥

105Hakika wanazua uongo tu wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waongo.

مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ﴿١٠٦

106Anayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini yule aliyekifungulia kifua chake ukafiri - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao wana adhabu kubwa.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ﴿١٠٧

107Hayo ni kwa sababu wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri.

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ﴿١٠٨

108Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na kusikia kwao na kuona kwao. Na hao ndio walioghafilika.

لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ﴿١٠٩

109Hakuna shaka ya kwamba hao ndio waliohasirika.

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا فُتِنُواْ ثُمَّ جَٰهَدُواْ وَصَبَرُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ﴿١١٠

110Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale waliohama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

۞ يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ﴿١١١

111Siku ambayo kila nafsi itakuja ikijitetea, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyotenda, nao hawatadhulumiwa.

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا قَرۡيَةٗ كَانَتۡ ءَامِنَةٗ مُّطۡمَئِنَّةٗ يَأۡتِيهَا رِزۡقُهَا رَغَدٗا مِّن كُلِّ مَكَانٖ فَكَفَرَتۡ بِأَنۡعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلۡجُوعِ وَٱلۡخَوۡفِ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ﴿١١٢

112Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa wingi kutokea kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvisha vazi la njaa na hofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.

وَلَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡهُمۡ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ﴿١١٣

113Na alikwishawajia Mjumbe kutoka miongoni mwao. Lakini wakamkadhibisha; basi ikawachukua adhabu hali ya kuwa ni madhalimu.

فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ﴿١١٤

114Basi kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ﴿١١٥

115Hakika amewaharimishia tu nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi, wala kuvuka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ﴿١١٦

116Wala msiseme uongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki ni halali, na hiki ni haramu - mkimzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafaulu.

مَتَٰعٞ قَلِيلٞ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ﴿١١٧

117Ni starehe ndogo tu, nao wana adhabu chungu.

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ﴿١١٨

118Na Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyokuhadithia zamani. Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe.

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ﴿١١٩

119Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa wale waliotenda mabaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mazuri; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةٗ قَانِتٗا لِّلَّهِ حَنِيفٗا وَلَمۡ يَكُ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ﴿١٢٠

120Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

شَاكِرٗا لِّأَنۡعُمِهِۚ ٱجۡتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ﴿١٢١

121Mwenye kuzishukuru neema zake. Yeye alimteua, na akamwongoa kwenye njia iliyonyooka.

وَءَاتَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ﴿١٢٢

122Na tukampa mazuri katika dunia, naye hakika Akhera atakuwa miongoni mwa walio wema.

ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ﴿١٢٣

123Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ﴿١٢٤

124Hakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa wale waliohitilafiana kuhusiana nayo. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.

ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ﴿١٢٥

125Lingania kwenye njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri zaidi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka.

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ﴿١٢٦

126Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri.

وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ﴿١٢٧

127Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Wala usiwahuzunikie, wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya njama wanazozifanya.

إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ﴿١٢٨

128Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na wale watendao mazuri.

RELATED SURAHS