Al-Fatiha

الفاتحة

The Opening7 ayahsMeccan

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ﴿١

1Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٢

2Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.[1]

ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ﴿٣

3Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.[1]

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ﴿٤

4Mmiliki wa Siku ya Malipo.

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ﴿٥

5Ni Wewe tu tunayeabudu, na ni Wewe tu tunayeomba msaada.

ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ﴿٦

6Tuongoe kwenye njia iliyonyooka.

صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ﴿٧

7Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea.

RELATED SURAHS