Al-Waqi'ah

الواقعة

The Event96 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ﴿١

1Litakapotokea hilo Tukio.

لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ﴿٢

2Hapana cha kukanusha kutokea kwake.

خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ﴿٣

3Literemshalo linyanyualo.

إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا﴿٤

4Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso.

وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا﴿٥

5Na milima itakaposagwasagwa.

فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا﴿٦

6Basi iwe mavumbi yanayopeperushwa.

وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ﴿٧

7Na nyinyi mtakuwa namna tatu.

فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ﴿٨

8Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ﴿٩

9Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?

وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ﴿١٠

10Na wa mbele watakuwa mbele.

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ﴿١١

11Hao ndio watakaowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu).

فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ﴿١٢

12Katika Bustani zenye neema.

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٣

13Fungu kubwa katika wa mwanzo.

وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ﴿١٤

14Na wachache katika wa mwisho.

عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ﴿١٥

15Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa.

مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ﴿١٦

16Wakiviegemea wakielekeana.

يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ﴿١٧

17Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele.

بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ﴿١٨

18Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchemi safi.

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ﴿١٩

19Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.

وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ﴿٢٠

20Na matunda wayapendayo.

وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ﴿٢١

21Na nyama za ndege kama wanavyotamani.

وَحُورٌ عِينٞ﴿٢٢

22Na Mahurulaini.

كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ﴿٢٣

23Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.

جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ﴿٢٤

24Ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda.

لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا﴿٢٥

25Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi.

إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا﴿٢٦

26Isipokuwa maneno ya Salama, Salama.

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ﴿٢٧

27Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?

فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ﴿٢٨

28Katika mikunazi isiyo na miba.

وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ﴿٢٩

29Na migomba iliyopangiliwa.

وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ﴿٣٠

30Na kivuli kilichotanda.

وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ﴿٣١

31Na maji yanayomiminika.

وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ﴿٣٢

32Na matunda mengi.

لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ﴿٣٣

33Hayatindikii wala hayakatazwi.

وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ﴿٣٤

34Na matandiko yaliyonyanyuliwa.

إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ﴿٣٥

35Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya.

فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا﴿٣٦

36Na tutawafanya vijana.

عُرُبًا أَتۡرَابٗا﴿٣٧

37Wanapendana na waume zao, hirimu moja.

لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ﴿٣٨

38Kwa ajili ya watu wa kuliani.

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿٣٩

39Fungu kubwa katika wa mwanzo.

وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ﴿٤٠

40Na fungu kubwa katika wa mwisho.

وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ﴿٤١

41Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?

فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ﴿٤٢

42Katika upepo wa moto, na maji yanayochemka.

وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ﴿٤٣

43Na kivuli cha moshi mweusi.

لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ﴿٤٤

44Si baridi wala cha kustarehesha.

إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ﴿٤٥

45Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.

وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ﴿٤٦

46Na walikuwa wakiendelea tu kufanya madhambi makubwa.

وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ﴿٤٧

47Na walikuwa wakisema: 'Tutakapokufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndiyo tutafufuliwa?

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ﴿٤٨

48Au baba zetu wa zamani?'

قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ﴿٤٩

49Sema: 'Hakika wa zamani na wa mwisho.'

لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ﴿٥٠

50Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.

ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ﴿٥١

51Kisha nyinyi, mliopotea, mnaokanusha.

لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ﴿٥٢

52Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.

فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ﴿٥٣

53Na kwa mti huo mtajaza matumbo.

فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ﴿٥٤

54Na juu yake mtakunywa maji yanayochemka.

فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ﴿٥٥

55Tena mtakunywa kama wanavyokunywa ngamia wenye kiu.

هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ﴿٥٦

56Hiyo ndiyo karamu yao ya kuwakaribisha Siku ya Malipo.

نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ﴿٥٧

57Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ﴿٥٨

58Je, mnaiona mbegu ya uzazi mnayoidondokesha?

ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ﴿٥٩

59Je, mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?

نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ﴿٦٠

60Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi.

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ﴿٦١

61Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilolijua.

وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ﴿٦٢

62Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ﴿٦٣

63Je, mnaona hivyo mnavyovipanda?

ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ﴿٦٤

64Je, ni nyinyi mnayoyaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?

لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ﴿٦٥

65Tungelitaka, tungeliyafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu.

إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ﴿٦٦

66Mkisema: 'Hakika sisi tumegharimika.'

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ﴿٦٧

67Bali sisi tumenyimwa.

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ﴿٦٨

68Je, mnayaona maji mnayoyanywa?

ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ﴿٦٩

69Je, ni nyinyi mnaoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?

لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ﴿٧٠

70Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ﴿٧١

71Je, mnauona moto mnaouwasha?

ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ﴿٧٢

72Ni nyinyi mliouumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?

نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ﴿٧٣

73Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ﴿٧٤

74Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.

۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ﴿٧٥

75Basi ninaapa kwa maanguko ya nyota.

وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ﴿٧٦

76Na hakika bila ya shaka hiki ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!

إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ﴿٧٧

77Hakika hii bila ya shaka ni Qur-ani Tukufu.

فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ﴿٧٨

78Katika Kitabu kilichohifadhiwa.

لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ﴿٧٩

79Hapana akigusaye ila waliotakaswa.

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٨٠

80Ni uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ﴿٨١

81Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?

وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ﴿٨٢

82Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?

فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ﴿٨٣

83Yawaje basi itakapofika roho kwenye koo.

وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ﴿٨٤

84Na nyinyi wakati huo mnatazama!

وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ﴿٨٥

85Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi, lakini hamuoni.

فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ﴿٨٦

86Na lau kuwa nyinyi hamtalipwa.

تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ﴿٨٧

87Kwa nini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?

فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ﴿٨٨

88Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu.

فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ﴿٨٩

89Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ﴿٩٠

90Na akiwa katika wale wa upande wa kulia.

فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ﴿٩١

91Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa wale wa upande wa kulia.

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ﴿٩٢

92Na ama akiwa katika wale waliokadhibisha, wapotovu.

فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ﴿٩٣

93Basi karamu ya makaribisho yake ni maji yanayochemka.

وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ﴿٩٤

94Na kutiwa Motoni.

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ﴿٩٥

95Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ﴿٩٦

96Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.

RELATED SURAHS