At-Takwir

التكوير

The Overthrowing29 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ﴿١

1Jua litakapokunjwa,

وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ﴿٢

2Na nyota zikazimwa,

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ﴿٣

3Na milima ikaondolewa,

وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ﴿٤

4Na ngamia wenye mimba pevu watakapoachwa wasishughulikiwe,

وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ﴿٥

5Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ﴿٦

6Na bahari zikawaka moto,

وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ﴿٧

7Na nafsi zikaunganishwa,

وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ﴿٨

8Na msichana aliyezikwa hai atakapoulizwa,

بِأَيِّ ذَنۢبٖ قُتِلَتۡ﴿٩

9Kwa kosa gani aliuliwa?

وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ﴿١٠

10Na madaftari yatakapoenezwa,

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ﴿١١

11Na mbingu itakapotanduliwa,

وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ﴿١٢

12Na Jahannamu itakapochochewa,

وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ﴿١٣

13Na Bustani ya mbinguni ikasongezwa karibu,

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ﴿١٤

14Kila nafsi itajua ilichokihudhurisha.

فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ﴿١٥

15Ninaapa kwa nyota zinaporejea nyuma.

ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ﴿١٦

16Zinazokwenda, kisha zikajificha.

وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ﴿١٧

17Na kwa usiku unapopungua.

وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ﴿١٨

18Na kwa asubuhi inapopambazuka.

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ﴿١٩

19Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu.

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ﴿٢٠

20Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi.

مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ﴿٢١

21Anayetiiwa, tena muaminifu.

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٖ﴿٢٢

22Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.

وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ﴿٢٣

23Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.

وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٖ﴿٢٤

24Wala yeye si bahili kwa mambo ya ghaibu.

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٖ﴿٢٥

25Wala hii si kauli ya Shetani aliyelaaniwa.

فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ﴿٢٦

26Basi mnakwenda wapi?

إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ﴿٢٧

27Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ﴿٢٨

28Kwa yule miongoni mwenu anayetaka kwenda sawa.

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٢٩

29Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

RELATED SURAHS