Al-Infitar

الانفطار

The Cleaving19 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ﴿١

1Mbingu itakapochanika.

وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ﴿٢

2Na nyota zitakapotawanyika.

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ﴿٣

3Na bahari zitakapopasuliwa.

وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ﴿٤

4Na makaburi yatakapofukuliwa.

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ﴿٥

5Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilichobakisha nyuma.

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ﴿٦

6Ewe mwanadamu! Nini kilichokudanganya ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?

ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ﴿٧

7Aliyekuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha.

فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ﴿٨

8Katika sura yoyote aliyoipenda akakujenga.

كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ﴿٩

9Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.

وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ﴿١٠

10Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu.

كِرَامٗا كَٰتِبِينَ﴿١١

11Waandishi wenye heshima.

يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ﴿١٢

12Wanayajua mnayoyatenda.

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ﴿١٣

13Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema.

وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ﴿١٤

14Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni.

يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ﴿١٥

15Wataingia humo Siku ya Malipo.

وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ﴿١٦

16Na hawatoacha kuwamo humo.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ﴿١٧

17Na nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani?

ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ﴿١٨

18Tena nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani?

يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ﴿١٩

19Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi nyingine; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.

RELATED SURAHS