الزلزلة
The Earthquake • 8 ayahs • Medinan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
2Na itakapotoa ardhi mizigo yake!
3Na mtu akasema: "Ina nini?"
4Siku hiyo itahadithia habari zake.
5Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
6Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
7Basi anayetenda chembe ya wema, atauona!
8Na anayetenda chembe ya uovu, atauona!