Al-'Adiyat

العاديات

The Chargers11 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا﴿١

1Ninaapa kwa farasi waendao mbio wakipumua.

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا﴿٢

2Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini.

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا﴿٣

3Wakishambulia wakati wa asubuhi.

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا﴿٤

4Huku wakitimua vumbi.

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا﴿٥

5Na wakijitoma kati ya kundi.

إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٞ﴿٦

6Hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!

وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٞ﴿٧

7Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!

وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ﴿٨

8Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!

۞ أَفَلَا يَعۡلَمُ إِذَا بُعۡثِرَ مَا فِي ٱلۡقُبُورِ﴿٩

9Kwani hajui watakapofufuliwa waliomo makaburini?

وَحُصِّلَ مَا فِي ٱلصُّدُورِ﴿١٠

10Na yakakusanywa yaliyomo vifuani?

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّخَبِيرُۢ﴿١١

11Hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na habari zao wote!

RELATED SURAHS