Al-Qari'ah

القارعة

The Striking Calamity11 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡقَارِعَةُ﴿١

1Inayogonga!

مَا ٱلۡقَارِعَةُ﴿٢

2Ni nini inayogonga?

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ﴿٣

3Na ni nini kitachokujulisha ni nini inayogonga?

يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ﴿٤

4Siku ambayo watu watakuwa kama nondo waliotawanywa;

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ﴿٥

5Na milima itakuwa kama sufu zilizochambuliwa!

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ﴿٦

6Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ﴿٧

7Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.

وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ﴿٨

8Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu.

فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ﴿٩

9Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ﴿١٠

10Na ni nini kitachokujulisha ni nini hiyo?

نَارٌ حَامِيَةُۢ﴿١١

11Ni Moto mkali!

RELATED SURAHS