التكاثر
The Rivalry in Worldly Increase • 8 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Kumekushughulisheni kutafuta wingi.
2Mpaka mkaja makaburini!
3Sivyo hivyo! Mtakujajua!
4Tena sivyo hivyo! Mtakujajua!
5Sivyo hivyo! Lau mngelijua kwa elimu ya yakini.
6Basi bila ya shaka mtaiona Jahiimu!
7Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
8Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema zote.