البينة
The Clear Proof • 8 ayahs • Medinan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache waliyo nayo mpaka iwajie bayana.
2Yaani Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakasika.
3Ndani yake mna maandiko yaliyonyooka.
4Wala hawakufarikiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.
5Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
6Hakika waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
7Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.
8Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za mbinguni za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi.