القدر
The Power • 5 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu).
2Na nini kitachokujulisha nini Laylatul Qadri?
3Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
4Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
5Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.