الضحى
The Morning Hours • 11 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Ninaapa kwa wakati wa kabla ya adhuhuri!
2Na kwa usiku unapotanda!
3Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
4Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia.
5Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
6Kwani hakukukuta yatima, akakupa makazi?
7Na akakukuta umepotea, akakuongoa?
8Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
9Basi yatima usimwonee!
10Na anayeomba au kuuliza usimkaripie!
11Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.