الليل
The Night • 21 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Ninaapa kwa usiku unapofunika!
2Na mchana unapodhihiri!
3Na kwa aliyeumba dume na jike!
4Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
5Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu.
6Na akalisadiki lililo jema.
7Tutamrahisishia yawe mepesi.
8Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake.
9Na akakanusha lililo jema.
10Tutamrahisishia yawe mazito!
11Na mali yake itamfaa nini atakapokuwa anadidimia?
12Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu.
13Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
14Basi nakuonyeni kutokana na Moto unaowaka vikali.
15Hatauingia ila mwovu kabisa!
16Anayekadhibisha na akageuka na kwenda zake.
17Na mcha Mungu ataepushwa nao.
18Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
19Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndiyo anamlipa.
20Ila ni kutaka uso wa Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
21Naye atakujaridhia!