Al-'Alaq

العلق

The Clot19 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ﴿١

1Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba.

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ﴿٢

2Amemuumba binaadamu kwa tone la damu.

ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ﴿٣

3Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!

ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ﴿٤

4Ambaye amefundisha kwa kalamu.

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ﴿٥

5Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.

كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ﴿٦

6Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.

أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ﴿٧

7Akijiona katajirika.

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ﴿٨

8Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ﴿٩

9Umemuona yule anayemkataza.

عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ﴿١٠

10Mja anaposali?

أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ﴿١١

11Umeona kama yeye yuko juu ya uongofu?

أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ﴿١٢

12Au anaamrisha ucha Mungu?

أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ﴿١٣

13Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?

أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ﴿١٤

14Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?

كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ﴿١٥

15Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!

نَاصِيَةٖ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٖ﴿١٦

16Shungi la uongo, lenye makosa!

فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ﴿١٧

17Basi na awaite wenzake!

سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ﴿١٨

18Nasi tutawaita Mazabania!

كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩﴿١٩

19Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!

RELATED SURAHS