Al-Mutaffifin

المطففين

The Defrauders36 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ﴿١

1Ole wao hao wapunjao!

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ﴿٢

2Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ﴿٣

3Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ﴿٤

4Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa.

لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ﴿٥

5Katika Siku iliyo kuu.

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٦

6Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ﴿٧

7Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ﴿٨

8Unajua nini Sijjin?

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ﴿٩

9Kitabu kilichoandikwa.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿١٠

10Ole wao siku hiyo kwa wanaokadhibisha!

ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ﴿١١

11Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ﴿١٢

12Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٣

13Anaposomewa Aya zetu husema: "Ni visa vya watu wa kale!"

كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ﴿١٤

14Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma.

كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ﴿١٥

15Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa mbali na neema za Mola wao Mlezi.

ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ﴿١٦

16Kisha wataingia Motoni!

ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ﴿١٧

17Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhibisha.

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ﴿١٨

18Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika Illiyyin.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ﴿١٩

19Na nini kitakachokujuvya nini Iliyyin?

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ﴿٢٠

20Kitabu kilichoandikwa.

يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ﴿٢١

21Wanakishuhudia waliokaribishwa.

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ﴿٢٢

22Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ﴿٢٣

23Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.

تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ﴿٢٤

24Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,

يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ﴿٢٥

25Watanyweshwa kinywaji safi kilichozibwa vyema.

خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ﴿٢٦

26Kizibo chake ni miski. Na katika hayo na washindanie wenye kushindana.

وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ﴿٢٧

27Na mchanganyiko wake ni Tasniim.

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ﴿٢٨

28Chemchemi watakayoinywa waliokurubishwa.

إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ﴿٢٩

29Kwa hakika wale waliokuwa wahalifu walikuwa wakiwacheka walioamini.

وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ﴿٣٠

30Na wanapopita karibu yao wakikonyezana.

وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ﴿٣١

31Na wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.

وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ﴿٣٢

32Na wanapowaona husema: Hakika hawa ndio hasa waliopotea.

وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ﴿٣٣

33Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.

فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ﴿٣٤

34Basi leo walioamini ndio watawacheka makafiri.

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ﴿٣٥

35Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.

هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ﴿٣٦

36Je, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?

RELATED SURAHS