الانشقاق
The Splitting Open • 25 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Itakapochanika mbingu.
2Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.
3Na ardhi itakapotanuliwa.
4Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu.
5Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.
6Ewe mtu! Hakika wewe unafanya matendo kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
7Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia.
8Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi.
9Na arudi kwa ahali zake na furaha.
10Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake.
11Basi huyo ataomba kuteketea.
12Na ataingia Motoni.
13Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
14Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
15Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona vyema!
16Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapokuchwa.
17Na kwa usiku na unavyovikusanya.
18Na kwa mwezi unapopevuka.
19Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka!
20Basi wana nini hawaamini?
21Na wanaposomewa Qur-ani hawasujudu?
22Bali waliokufuru wanakanusha tu.
23Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria.
24Basi wabashirie adhabu chungu!
25Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.