Al-Buruj

البروج

The Great Stars22 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ﴿١

1Ninaapa kwa mbingu yenye nyota kubwa kubwa!

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ﴿٢

2Na kwa Siku iliyoahidiwa!

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ﴿٣

3Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ﴿٤

4Wameangamizwa watu wa makhandaki.

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ﴿٥

5Yenye moto wenye kuni nyingi.

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ﴿٦

6Walipokuwa wamekaa hapo.

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ﴿٧

7Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini.

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ﴿٨

8Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ﴿٩

9Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ﴿١٠

10Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ﴿١١

11Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani za mbinguni zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ﴿١٢

12Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ﴿١٣

13Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejesha tena.

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ﴿١٤

14Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi.

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ﴿١٥

15Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu.

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٦

16Atendaye ayatakayo.

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ﴿١٧

17Je! Zimekufikia habari za Majeshi?

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ﴿١٨

18Ya Firauni na Thamudi?

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ﴿١٩

19Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha.

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ﴿٢٠

20Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ﴿٢١

21Bali hii ni Qur-ani tukufu.

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ﴿٢٢

22Katika Ubao uliohifadhiwa.

RELATED SURAHS