At-Tariq

الطارق

The Night Comer17 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ﴿١

1Ninaapa kwa mbingu na kinachokuja usiku!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ﴿٢

2Na nini kitakachokujulisha ni nini hicho kinachokuja usiku?

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ﴿٣

3Ni Nyota yenye mwanga mkali.

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ﴿٤

4Hapana nafsi ila inaye mwangalizi.

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ﴿٥

5Hebu na ajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani?

خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ﴿٦

6Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa.

يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ﴿٧

7Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.

إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ﴿٨

8Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.

يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ﴿٩

9Siku zitakapodhihirishwa siri.

فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ﴿١٠

10Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ﴿١١

11Ninaapa kwa mbingu yenye marejeo!

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ﴿١٢

12Na kwa ardhi inayopasuka!

إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ﴿١٣

13Hakika hii ni kauli ya kupambanua.

وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ﴿١٤

14Wala si mzaha.

إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا﴿١٥

15Hakika wao wanapanga mpango.

وَأَكِيدُ كَيۡدٗا﴿١٦

16Na Mimi napanga mpango.

فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا﴿١٧

17Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.

RELATED SURAHS