Al-A'la

الأعلى

The Most High19 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى﴿١

1Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa.

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ﴿٢

2Aliyeumba, na akaweka sawa.

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ﴿٣

3Na ambaye amekadiria na akaongoa.

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ﴿٤

4Na aliyeotesha malisho.

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ﴿٥

5Kisha akayafanya makavu, meusi.

سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ﴿٦

6Tutakusomesha wala hutasahau.

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ﴿٧

7Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana.

وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ﴿٨

8Na tutakusahilishia yawe mepesi.

فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ﴿٩

9Basi kumbusha, kama makumbusho yanafaa.

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ﴿١٠

10Atakumbuka mwenye kuogopa.

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى﴿١١

11Na atajitenga mbali nayo mpotovu.

ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ﴿١٢

12Ambaye atauingia Moto mkubwa.

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ﴿١٣

13Tena humo hatakufa wala hawi hai.

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ﴿١٤

14Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa.

وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ﴿١٥

15Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.

بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا﴿١٦

16Lakini nyinyi mnapendelea maisha ya dunia!

وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ﴿١٧

17Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ﴿١٨

18Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo.

صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ﴿١٩

19Vitabu vya Ibrahimu na Musa.

RELATED SURAHS