Al-Ghashiyah

الغاشية

The Overwhelming26 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ﴿١

1Je, imekufikia habari ya Msiba wa kufudikiza?

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ﴿٢

2Siku hiyo nyuso zitainama.

عَامِلَةٞ نَّاصِبَةٞ﴿٣

3Zikifanya kazi, nazo taabani.

تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةٗ﴿٤

4Ziingie katika Moto unaowaka.

تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٖ﴿٥

5Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka.

لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٖ﴿٦

6Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba.

لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٖ﴿٧

7Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاعِمَةٞ﴿٨

8Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.

لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٞ﴿٩

9Zitakuwa radhi kwa juhudi yao.

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ﴿١٠

10Katika Bustani ya juu.

لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةٗ﴿١١

11Hawatasikia humo upuuzi.

فِيهَا عَيۡنٞ جَارِيَةٞ﴿١٢

12Humo imo chemchemi inayomiminika.

فِيهَا سُرُرٞ مَّرۡفُوعَةٞ﴿١٣

13Humo vimo viti vilivyonyanyuliwa.

وَأَكۡوَابٞ مَّوۡضُوعَةٞ﴿١٤

14Na bilauri zilizopangwa.

وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةٞ﴿١٥

15Na matakia safu safu.

وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ﴿١٦

16Na mazulia yaliyotandikwa.

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ﴿١٧

17Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa?

وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ﴿١٨

18Na mbingu jinsi ilivyoinuliwa?

وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ﴿١٩

19Na milima jinsi ilivyowekwa imara?

وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ﴿٢٠

20Na ardhi jinsi ilivyotandazwa?

فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٞ﴿٢١

21Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.

لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ﴿٢٢

22Wewe si mwenye kuwatawalia.

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ﴿٢٣

23Lakini anayerudi nyuma na kukataa.

فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ﴿٢٤

24Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!

إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ﴿٢٥

25Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم﴿٢٦

26Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!

RELATED SURAHS