Al-Fajr

الفجر

The Dawn30 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡفَجۡرِ﴿١

1Ninaapa kwa alfajiri.

وَلَيَالٍ عَشۡرٖ﴿٢

2Na kwa masiku kumi.

وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ﴿٣

3Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ﴿٤

4Na kwa usiku unapopita.

هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ﴿٥

5Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ﴿٦

6Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di?

إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ﴿٧

7Wa Iram, wenye majumba marefu?

ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ﴿٨

8Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?

وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ﴿٩

9Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?

وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ﴿١٠

10Na Firauni mwenye vigingi?

ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ﴿١١

11Ambao walifanya jeuri katika nchi?

فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ﴿١٢

12Wakakithirisha humo ufisadi?

فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ﴿١٣

13Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.

إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ﴿١٤

14Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.

فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ﴿١٥

15Ama mtu anapojaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!

وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ﴿١٦

16Na ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!

كَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ﴿١٧

17Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima.

وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ﴿١٨

18Wala hamhimizani kulisha masikini.

وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا﴿١٩

19Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa.

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا﴿٢٠

20Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.

كَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكّٗا دَكّٗا﴿٢١

21Sivyo hivyo! Itakapovunjwa ardhi vipande vipande.

وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفّٗا صَفّٗا﴿٢٢

22Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu.

وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٖ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ﴿٢٣

23Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?

يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي﴿٢٤

24Atasema: Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu!

فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٞ﴿٢٥

25Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٞ﴿٢٦

26Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.

يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ﴿٢٧

27Ewe nafsi iliyotua!

ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةٗ مَّرۡضِيَّةٗ﴿٢٨

28Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umeridhiwa.

فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي﴿٢٩

29Basi ingia miongoni mwa waja wangu.

وَٱدۡخُلِي جَنَّتِي﴿٣٠

30Na ingia katika Bustani yangu.

RELATED SURAHS