Al-Balad

البلد

The City20 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ﴿١

1Ninaapa kwa Mji huu!

وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ﴿٢

2Nawe unaukaa Mji huu.

وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ﴿٣

3Na ninaapa kwa mzazi na alichokizaa.

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ﴿٤

4Hakika tumemuumba mtu katika taabu.

أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ﴿٥

5Ati anadhani hapana yeyote atakayemuweza?

يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا﴿٦

6Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.

أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ﴿٧

7Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anayemwona?

أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ﴿٨

8Kwani hatukumpa macho mawili?

وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ﴿٩

9Na ulimi, na midomo miwili?

وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ﴿١٠

10Na tukambainishia zote njia mbili?

فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ﴿١١

11Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ﴿١٢

12Na nini kitakachokujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?

فَكُّ رَقَبَةٍ﴿١٣

13Kumkomboa mtumwa.

أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ﴿١٤

14Au kumlisha siku ya njaa,

يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ﴿١٥

15Yatima aliye jamaa.

أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ﴿١٦

16Au masikini aliye vumbini.

ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ﴿١٧

17Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.

أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ﴿١٨

18Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ﴿١٩

19Lakini waliozikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.

عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ﴿٢٠

20Juu yao utakuwa Moto uliofungiwa kila upande.

RELATED SURAHS