As-Saffat

الصافات

Those Ranged in Ranks182 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفّٗا﴿١

1Ninaapa kwa wanaojipanga kwa safu.

فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجۡرٗا﴿٢

2Na kwa wenye kukataza mabaya.

فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا﴿٣

3Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.

إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدٞ﴿٤

4Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.

رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ﴿٥

5Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yake, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.

إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ﴿٦

6Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.

وَحِفۡظٗا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ مَّارِدٖ﴿٧

7Na kulinda na kila shetani muasi.

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٖ﴿٨

8Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.

دُحُورٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ وَاصِبٌ﴿٩

9Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.

إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ ثَاقِبٞ﴿١٠

10Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinachong'ara.

فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينٖ لَّازِبِۭ﴿١١

11Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.

بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ﴿١٢

12Bali unastaajabu, na wao wanafanya masihara.

وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ﴿١٣

13Na wanapokumbushwa, hawakumbuki.

وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةٗ يَسۡتَسۡخِرُونَ﴿١٤

14Na wanapoona Ishara, wanafanya masihara.

وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٌ﴿١٥

15Na husema: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi tu ulio dhahiri.

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ﴿١٦

16Ati tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ﴿١٧

17Hata baba zetu wa zamani?

قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ﴿١٨

18Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ﴿١٩

19Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndipo wataona!

وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ﴿٢٠

20Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.

هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ﴿٢١

21Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyokuwa mkiikadhibisha.

۞ ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ﴿٢٢

22Wakusanyeni wale waliodhulumu, na wote walio mfano wao, na hao ambao wao walikuwa wakiwaabudu.

مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ﴿٢٣

23Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!

وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ﴿٢٤

24Na wasimamisheni. Hakika hao wataulizwa:

مَا لَكُمۡ لَا تَنَاصَرُونَ﴿٢٥

25Mna nini? Mbona hamsaidiani?

بَلۡ هُمُ ٱلۡيَوۡمَ مُسۡتَسۡلِمُونَ﴿٢٦

26Bali hii leo, watasalimu amri.

وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ﴿٢٧

27Wataelekeana wao kwa wao kuulizana.

قَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَأۡتُونَنَا عَنِ ٱلۡيَمِينِ﴿٢٨

28Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.

قَالُواْ بَل لَّمۡ تَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ﴿٢٩

29Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.

وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭۖ بَلۡ كُنتُمۡ قَوۡمٗا طَٰغِينَ﴿٣٠

30Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.

فَحَقَّ عَلَيۡنَا قَوۡلُ رَبِّنَآۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ﴿٣١

31Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.

فَأَغۡوَيۡنَٰكُمۡ إِنَّا كُنَّا غَٰوِينَ﴿٣٢

32Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.

فَإِنَّهُمۡ يَوۡمَئِذٖ فِي ٱلۡعَذَابِ مُشۡتَرِكُونَ﴿٣٣

33Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ﴿٣٤

34Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wahalifu.

إِنَّهُمۡ كَانُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسۡتَكۡبِرُونَ﴿٣٥

35Wao walipokuwa wakiambiwa, "La ilaha illallaahu (Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu)", wanajivuna.

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓاْ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٖ مَّجۡنُونِۭ﴿٣٦

36Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?

بَلۡ جَآءَ بِٱلۡحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿٣٧

37Bali huyu amekuja kwa haki, na amewasadikisha Mitume.

إِنَّكُمۡ لَذَآئِقُواْ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡأَلِيمِ﴿٣٨

38Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.

وَمَا تُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ﴿٣٩

39Wala hamlipwi isipokuwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ﴿٤٠

40Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu walioteuliwa.

أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ رِزۡقٞ مَّعۡلُومٞ﴿٤١

41Hao ndio watakaopata riziki maalumu.

فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكۡرَمُونَ﴿٤٢

42Matunda, nao wataheshimiwa.

فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ﴿٤٣

43Katika Bustani za neema.

عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ﴿٤٤

44Wako juu ya viti mfano wa kitanda wameelekeana.

يُطَافُ عَلَيۡهِم بِكَأۡسٖ مِّن مَّعِينِۭ﴿٤٥

45Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchemi.

بَيۡضَآءَ لَذَّةٖ لِّلشَّٰرِبِينَ﴿٤٦

46Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.

لَا فِيهَا غَوۡلٞ وَلَا هُمۡ عَنۡهَا يُنزَفُونَ﴿٤٧

47Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.

وَعِندَهُمۡ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ عِينٞ﴿٤٨

48Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri.

كَأَنَّهُنَّ بَيۡضٞ مَّكۡنُونٞ﴿٤٩

49Hao wanawake kama mayai yaliyohifadhika.

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ﴿٥٠

50Basi wakaelekeana kuulizana wenyewe kwa wenyewe.

قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٞ﴿٥١

51Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki.

يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُصَدِّقِينَ﴿٥٢

52Aliyekuwa akiniambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki.

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ﴿٥٣

53Ati tukishakufa tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kufanyiwa hesabu?

قَالَ هَلۡ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ﴿٥٤

54Atasema: Je, nyie mnawaona?

فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِي سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ﴿٥٥

55Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.

قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرۡدِينِ﴿٥٦

56Atasema: Wallahi! (Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia sana kunipoteza.

وَلَوۡلَا نِعۡمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ﴿٥٧

57Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa.

أَفَمَا نَحۡنُ بِمَيِّتِينَ﴿٥٨

58Je, sisi hatutakufa?

إِلَّا مَوۡتَتَنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ﴿٥٩

59Isipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ﴿٦٠

60Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.

لِمِثۡلِ هَٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ ٱلۡعَٰمِلُونَ﴿٦١

61Kwa mfano wa haya na watende watendao.

أَذَٰلِكَ خَيۡرٞ نُّزُلًا أَمۡ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ﴿٦٢

62Je, kukaribishwa hivi si ndiyo bora, au mti wa Zaqqum?

إِنَّا جَعَلۡنَٰهَا فِتۡنَةٗ لِّلظَّٰلِمِينَ﴿٦٣

63Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa waliodhulumu.

إِنَّهَا شَجَرَةٞ تَخۡرُجُ فِيٓ أَصۡلِ ٱلۡجَحِيمِ﴿٦٤

64Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Jahannamu.

طَلۡعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَٰطِينِ﴿٦٥

65Mashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashetani.

فَإِنَّهُمۡ لَأٓكِلُونَ مِنۡهَا فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ﴿٦٦

66Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo kwayo.

ثُمَّ إِنَّ لَهُمۡ عَلَيۡهَا لَشَوۡبٗا مِّنۡ حَمِيمٖ﴿٦٧

67Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyochemka.

ثُمَّ إِنَّ مَرۡجِعَهُمۡ لَإِلَى ٱلۡجَحِيمِ﴿٦٨

68Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa Jahimu.

إِنَّهُمۡ أَلۡفَوۡاْ ءَابَآءَهُمۡ ضَآلِّينَ﴿٦٩

69Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.

فَهُمۡ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمۡ يُهۡرَعُونَ﴿٧٠

70Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.

وَلَقَدۡ ضَلَّ قَبۡلَهُمۡ أَكۡثَرُ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿٧١

71Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ﴿٧٢

72Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.

فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ﴿٧٣

73Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walioonywa.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ﴿٧٤

74Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

وَلَقَدۡ نَادَىٰنَا نُوحٞ فَلَنِعۡمَ ٱلۡمُجِيبُونَ﴿٧٥

75Na hakika Nuhu alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.

وَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ﴿٧٦

76Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.

وَجَعَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلۡبَاقِينَ﴿٧٧

77Na tuliwajaalia dhuria zake ndio wenye kubakia.

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ﴿٧٨

78Na tukamwachia (sifa njema) kwa waliokuja baadaye.

سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحٖ فِي ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٧٩

79Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿٨٠

80Kwa hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema.

إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿٨١

81Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ﴿٨٢

82Kisha tukawazamisha wale wengine.

۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٰهِيمَ﴿٨٣

83Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake.

إِذۡ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلۡبٖ سَلِيمٍ﴿٨٤

84Alipomjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.

إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ﴿٨٥

85Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?

أَئِفۡكًا ءَالِهَةٗ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ﴿٨٦

86Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٨٧

87Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?"

فَنَظَرَ نَظۡرَةٗ فِي ٱلنُّجُومِ﴿٨٨

88Kisha akapiga jicho kutazama nyota.

فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٞ﴿٨٩

89Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!

فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ﴿٩٠

90Nao wakamwacha, wakampa kisogo.

فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ﴿٩١

91Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?

مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ﴿٩٢

92Mna nini hata hamsemi?

فَرَاغَ عَلَيۡهِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ﴿٩٣

93Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.

فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ﴿٩٤

94Basi wakamjia upesi upesi.

قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ﴿٩٥

95Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe?

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ﴿٩٦

96Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya!

قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنٗا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ﴿٩٧

97Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!

فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدٗا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ﴿٩٨

98Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini zaidi.

وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ﴿٩٩

99Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.

رَبِّ هَبۡ لِي مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ﴿١٠٠

100Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.

فَبَشَّرۡنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمٖ﴿١٠١

101Basi tukambashiria mwana aliye mpole.

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعۡيَ قَالَ يَٰبُنَيَّ إِنِّيٓ أَرَىٰ فِي ٱلۡمَنَامِ أَنِّيٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفۡعَلۡ مَا تُؤۡمَرُۖ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ﴿١٠٢

102Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Insha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri.

فَلَمَّآ أَسۡلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلۡجَبِينِ﴿١٠٣

103Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.

وَنَٰدَيۡنَٰهُ أَن يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ﴿١٠٤

104Tulimwita: Ewe Ibrahim!

قَدۡ صَدَّقۡتَ ٱلرُّءۡيَآۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿١٠٥

105Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaotenda mema.

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡبَلَٰٓؤُاْ ٱلۡمُبِينُ﴿١٠٦

106Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri.

وَفَدَيۡنَٰهُ بِذِبۡحٍ عَظِيمٖ﴿١٠٧

107Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ﴿١٠٨

108Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye.

سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ﴿١٠٩

109Iwe salama kwa Ibrahim!

كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿١١٠

110Hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema.

إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿١١١

111Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

وَبَشَّرۡنَٰهُ بِإِسۡحَٰقَ نَبِيّٗا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ﴿١١٢

112Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.

وَبَٰرَكۡنَا عَلَيۡهِ وَعَلَىٰٓ إِسۡحَٰقَۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحۡسِنٞ وَظَالِمٞ لِّنَفۡسِهِۦ مُبِينٞ﴿١١٣

113Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuria zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.

وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ﴿١١٤

114Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.

وَنَجَّيۡنَٰهُمَا وَقَوۡمَهُمَا مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ﴿١١٥

115Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.

وَنَصَرۡنَٰهُمۡ فَكَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ﴿١١٦

116Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.

وَءَاتَيۡنَٰهُمَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلۡمُسۡتَبِينَ﴿١١٧

117Na tukawapa wawili hao Kitabu kinachobainisha.

وَهَدَيۡنَٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ﴿١١٨

118Na tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka.

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِمَا فِي ٱلۡأٓخِرِينَ﴿١١٩

119Na tukawaachia (sifa njema) katika watu waliokuja baadaye.

سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ﴿١٢٠

120Iwe salama kwa Musa na Haruni!

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿١٢١

121Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema.

إِنَّهُمَا مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿١٢٢

122Hakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini.

وَإِنَّ إِلۡيَاسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿١٢٣

123Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.

إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ﴿١٢٤

124Alipowaambia watu wake: Hamumchi Mungu?

أَتَدۡعُونَ بَعۡلٗا وَتَذَرُونَ أَحۡسَنَ ٱلۡخَٰلِقِينَ﴿١٢٥

125Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji.

ٱللَّهَ رَبَّكُمۡ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٢٦

126Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?

فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ﴿١٢٧

127Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ﴿١٢٨

128Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ﴿١٢٩

129Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa waliokuja baadaye.

سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلۡ يَاسِينَ﴿١٣٠

130Iwe salama kwa Ilyas.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿١٣١

131Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema.

إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿١٣٢

132Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

وَإِنَّ لُوطٗا لَّمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿١٣٣

133Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.

إِذۡ نَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ﴿١٣٤

134Tulipomwokoa yeye na ahali zake wote.

إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ﴿١٣٥

135Isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma.

ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ﴿١٣٦

136Kisha tukawaangamiza wale wengineo.

وَإِنَّكُمۡ لَتَمُرُّونَ عَلَيۡهِم مُّصۡبِحِينَ﴿١٣٧

137Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi.

وَبِٱلَّيۡلِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ﴿١٣٨

138Na usiku. Basi je, hamyatii akilini?

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿١٣٩

139Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.

إِذۡ أَبَقَ إِلَى ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ﴿١٤٠

140Alipokimbia akenda katika jahazi lililosheheni.

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُدۡحَضِينَ﴿١٤١

141Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa.

فَٱلۡتَقَمَهُ ٱلۡحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٞ﴿١٤٢

142Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.

فَلَوۡلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُسَبِّحِينَ﴿١٤٣

143Na ingelikuwa hakuwa katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu.

لَلَبِثَ فِي بَطۡنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ﴿١٤٤

144Bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.

۞ فَنَبَذۡنَٰهُ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٞ﴿١٤٥

145Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.

وَأَنۢبَتۡنَا عَلَيۡهِ شَجَرَةٗ مِّن يَقۡطِينٖ﴿١٤٦

146Na tukauotesha juu yake mmea wa aina ya mung'unye.

وَأَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ مِاْئَةِ أَلۡفٍ أَوۡ يَزِيدُونَ﴿١٤٧

147Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.

فَـَٔامَنُواْ فَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٖ﴿١٤٨

148Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.

فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَلِرَبِّكَ ٱلۡبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلۡبَنُونَ﴿١٤٩

149Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?

أَمۡ خَلَقۡنَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِنَٰثٗا وَهُمۡ شَٰهِدُونَ﴿١٥٠

150Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?

أَلَآ إِنَّهُم مِّنۡ إِفۡكِهِمۡ لَيَقُولُونَ﴿١٥١

151Tazama, hakika ni kwa uzushi wao ndio wanasema.

وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ﴿١٥٢

152Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!

أَصۡطَفَى ٱلۡبَنَاتِ عَلَى ٱلۡبَنِينَ﴿١٥٣

153Ati amehiari watoto wa kike kuliko wanaume?

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ﴿١٥٤

154Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٥٥

155Hamkumbuki?

أَمۡ لَكُمۡ سُلۡطَٰنٞ مُّبِينٞ﴿١٥٦

156Au mnayo hoja iliyo wazi?

فَأۡتُواْ بِكِتَٰبِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ﴿١٥٧

157Basi leteni Kitabu chenu kama nyinyi ni wakweli.

وَجَعَلُواْ بَيۡنَهُۥ وَبَيۡنَ ٱلۡجِنَّةِ نَسَبٗاۚ وَلَقَدۡ عَلِمَتِ ٱلۡجِنَّةُ إِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ﴿١٥٨

158Na wameweka mahusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwishajua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.

سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿١٥٩

159Ametakasika Mwenyezi Mungu mbali na hayo wanayomsingizia.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ﴿١٦٠

160Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

فَإِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ﴿١٦١

161Basi hakika nyinyi na mnaowaabudu.

مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ بِفَٰتِنِينَ﴿١٦٢

162Hamwezi kuwapoteza.

إِلَّا مَنۡ هُوَ صَالِ ٱلۡجَحِيمِ﴿١٦٣

163Isipokuwa yule atakayeingia Motoni.

وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٞ مَّعۡلُومٞ﴿١٦٤

164Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.

وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلصَّآفُّونَ﴿١٦٥

165Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.

وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡمُسَبِّحُونَ﴿١٦٦

166Na hakika sisi ndio wenye kutakasa.

وَإِن كَانُواْ لَيَقُولُونَ﴿١٦٧

167Na walikuwapo waliokuwa wakisema.

لَوۡ أَنَّ عِندَنَا ذِكۡرٗا مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٦٨

168Tungelikuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani.

لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ﴿١٦٩

169Bila ya shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumkusudia Yeye tu.

فَكَفَرُواْ بِهِۦۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ﴿١٧٠

170Lakini waliukufuru. Basi watakuja jua.

وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿١٧١

171Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu waliotumwa.

إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ﴿١٧٢

172Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa.

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ﴿١٧٣

173Na kwamba jeshi letu ndilo litakaloshinda.

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ﴿١٧٤

174Basi waachilie mbali kwa muda.

وَأَبۡصِرۡهُمۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ﴿١٧٥

175Na watazame, nao wataona.

أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ﴿١٧٦

176Je, wanaiharakishia adhabu yetu?

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمۡ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلۡمُنذَرِينَ﴿١٧٧

177Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa.

وَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ﴿١٧٨

178Na waache kwa muda.

وَأَبۡصِرۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ﴿١٧٩

179Na tazama, na wao wataona.

سُبۡحَٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلۡعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿١٨٠

180Ametakasika Mola wako Mlezi Mwenye utukufu mbali na yale wanayomzulia.

وَسَلَٰمٌ عَلَى ٱلۡمُرۡسَلِينَ﴿١٨١

181Na Salamu juu ya Mitume.

وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿١٨٢

182Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

RELATED SURAHS