Ta-Ha

طه

Ta-Ha135 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

طه﴿١

1Twa Ha![1]

مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ﴿٢

2Hatukukuteremshia Qur-ani ili upate mashaka.

إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ﴿٣

3Bali ni ukumbusho kwa mwenye kunyenyekea.

تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى﴿٤

4Ni uteremsho kutoka kwa aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu.

ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ﴿٥

5Arrahmani (Mwingi wa rehema), aliyeinuka juu ya Kiti cha Enzi.

لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَمَا تَحۡتَ ٱلثَّرَىٰ﴿٦

6Ni vyake vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, na vilivyo baina yake, na vilivyo chini ya ardhi.

وَإِن تَجۡهَرۡ بِٱلۡقَوۡلِ فَإِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخۡفَى﴿٧

7Na ukinyanyua sauti kwa kusema, basi hakika Yeye anajua siri na chini zaidi kuliko siri.

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ﴿٨

8Mwenyezi Mungu! Hakuna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri zaidi.

وَهَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ﴿٩

9Na je, imekufikia hadithi ya Musa?

إِذۡ رَءَا نَارٗا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدٗى﴿١٠

10Alipouona moto, kwa hivyo akawaambia ahali zake: Ngojeni! Hakika mimi nimeuona moto, huenda nikawaletea kijinga kutoka humo, au nikapata uongofu kwenye moto huo.

فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ يَٰمُوسَىٰٓ﴿١١

11Basi alipoufikia, akaitwa: Ewe Musa!

إِنِّيٓ أَنَا۠ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوٗى﴿١٢

12Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani uko katika bonde takatifu la 'Tuwa.

وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ﴿١٣

13Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza yanayofunuliwa.

إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ﴿١٤

14Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hakuna mungu isipokuwa Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na udumishe Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ﴿١٥

15Hakika Saa itakuja bila ya shaka. Nimekaribia mno kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyoyafanya.

فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡهَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرۡدَىٰ﴿١٦

16Kwa hivyo, kamwe asikuzuilie nayo yule ambaye haiamini na akafuata matamanio yake ukaja kuangamia.

وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ﴿١٧

17Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?

قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ﴿١٨

18Akasema: Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani kwayo kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.

قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ﴿١٩

19Akasema: Itupe, ewe Musa!

فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ﴿٢٠

20Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio.

قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ﴿٢١

21Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.

وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ﴿٢٢

22Na uambatishe mkono wako kwenye ubavu, utatoka mweupe pasipo na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyingine.

لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى﴿٢٣

23Ili tukuonyeshe katika ishara zetu kubwa.

ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ﴿٢٤

24Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.

قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي﴿٢٥

25(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu.

وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي﴿٢٦

26Na nirahisishie kazi yangu hii.

وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي﴿٢٧

27Na lifungue fundo lililo katika ulimi wangu.

يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي﴿٢٨

28Wapate kufahamu maneno yangu.

وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي﴿٢٩

29Na nipe msaidizi katika ahali zangu.

هَٰرُونَ أَخِي﴿٣٠

30Harun, kaka yangu.

ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي﴿٣١

31Kwake yeye niongeze nguvu zangu.

وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي﴿٣٢

32Na mshirikishe katika jambo langu hili.

كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا﴿٣٣

33Ili tukutakase kwa wingi.

وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا﴿٣٤

34Na tukutaje kwa wingi.

إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا﴿٣٥

35Hakika Wewe unatuona vyema.

قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ﴿٣٦

36Akasema: Hakika Umeshapewa maombi yako, ewe Musa!

وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ﴿٣٧

37Na hakika tulikwishakufanyia hisani mara nyingine.

إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ﴿٣٨

38Pale tulipomfunulia mama yako yaliyofunuliwa,

أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوّٞ لِّي وَعَدُوّٞ لَّهُۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةٗ مِّنِّي وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِيٓ﴿٣٩

39Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayotoka kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.

إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ﴿٤٠

40Dada yako alipokwenda na akasema: Je! Niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuua mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa, ewe Musa!

وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِي﴿٤١

41Na nimekuteua kwa ajili ya nafsi yangu.

ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَٰتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكۡرِي﴿٤٢

42Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.

ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ﴿٤٣

43Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.

فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ﴿٤٤

44Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.

قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ﴿٤٥

45Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.

قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِي مَعَكُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ﴿٤٦

46Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.

فَأۡتِيَاهُ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَا تُعَذِّبۡهُمۡۖ قَدۡ جِئۡنَٰكَ بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكَۖ وَٱلسَّلَٰمُ عَلَىٰ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلۡهُدَىٰٓ﴿٤٧

47Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani iwe juu ya atakayefuata uongofu.

إِنَّا قَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡنَآ أَنَّ ٱلۡعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ﴿٤٨

48Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hakuna shaka adhabu itampata anayekadhibisha na akapuuza

قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَٰمُوسَىٰ﴿٤٩

49(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?

قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِيٓ أَعۡطَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ خَلۡقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ﴿٥٠

50Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.

قَالَ فَمَا بَالُ ٱلۡقُرُونِ ٱلۡأُولَىٰ﴿٥١

51Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?

قَالَ عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَٰبٖۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى﴿٥٢

52Akasema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau.

ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مَهۡدٗا وَسَلَكَ لَكُمۡ فِيهَا سُبُلٗا وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّن نَّبَاتٖ شَتَّىٰ﴿٥٣

53Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawapitishia humo njia, na akawateremshia kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbalimbali za mimea.

كُلُواْ وَٱرۡعَوۡاْ أَنۡعَٰمَكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ﴿٥٤

54Kuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wenye akili.

۞ مِنۡهَا خَلَقۡنَٰكُمۡ وَفِيهَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡهَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ﴿٥٥

55Tumewaumba kutokana nayo (ardhi), na humo tutawarudisha, na tutawatoa kutoka humo mara nyengine.

وَلَقَدۡ أَرَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ﴿٥٦

56Na hakika tulimwonyesha ishara zetu zote. Lakini alikadhibisha na akakataa.

قَالَ أَجِئۡتَنَا لِتُخۡرِجَنَا مِنۡ أَرۡضِنَا بِسِحۡرِكَ يَٰمُوسَىٰ﴿٥٧

57Akasema: Ewe Musa! Hivyo umetujia kututoa katika nchi yetu kwa uchawi wako?

فَلَنَأۡتِيَنَّكَ بِسِحۡرٖ مِّثۡلِهِۦ فَٱجۡعَلۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكَ مَوۡعِدٗا لَّا نُخۡلِفُهُۥ نَحۡنُ وَلَآ أَنتَ مَكَانٗا سُوٗى﴿٥٨

58Basi sisi hakika tutakuletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali patakapokuwa sawa.

قَالَ مَوۡعِدُكُمۡ يَوۡمُ ٱلزِّينَةِ وَأَن يُحۡشَرَ ٱلنَّاسُ ضُحٗى﴿٥٩

59Akasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu ya mapambo; na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.

فَتَوَلَّىٰ فِرۡعَوۡنُ فَجَمَعَ كَيۡدَهُۥ ثُمَّ أَتَىٰ﴿٦٠

60Basi Firauni akageuka akarudi, na akatengeneza hila yake, kisha akaja.

قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيۡلَكُمۡ لَا تَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا فَيُسۡحِتَكُم بِعَذَابٖۖ وَقَدۡ خَابَ مَنِ ٱفۡتَرَىٰ﴿٦١

61Musa akawaambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uongo, akaja kuwafutilia mbali kwa adhabu. Na hakika mwenye kuzua lazima ashindwe!

فَتَنَٰزَعُوٓاْ أَمۡرَهُم بَيۡنَهُمۡ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّجۡوَىٰ﴿٦٢

62Basi wakazozana wenyewe kwa wenyewe kuhusiana na jambo lao hilo, na wakanong'ona kwa siri.

قَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَٰنِ لَسَٰحِرَٰنِ يُرِيدَانِ أَن يُخۡرِجَاكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِمَا وَيَذۡهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ ٱلۡمُثۡلَىٰ﴿٦٣

63Wakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kuwatoa katika nchi yenu kwa uchawi wao, na waondoe mila zenu zilizo bora kabisa.

فَأَجۡمِعُواْ كَيۡدَكُمۡ ثُمَّ ٱئۡتُواْ صَفّٗاۚ وَقَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡيَوۡمَ مَنِ ٱسۡتَعۡلَىٰ﴿٦٤

64Kwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakayeshinda.

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَلۡقَىٰ﴿٦٥

65Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio wa kwanza wa kutupa?

قَالَ بَلۡ أَلۡقُواْۖ فَإِذَا حِبَالُهُمۡ وَعِصِيُّهُمۡ يُخَيَّلُ إِلَيۡهِ مِن سِحۡرِهِمۡ أَنَّهَا تَسۡعَىٰ﴿٦٦

66Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki! Kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinakwenda mbio.

فَأَوۡجَسَ فِي نَفۡسِهِۦ خِيفَةٗ مُّوسَىٰ﴿٦٧

67Basi Musa akaingia hofu katika nafsi yake.

قُلۡنَا لَا تَخَفۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡأَعۡلَىٰ﴿٦٨

68Tukasema: Usihofu! Hakika wewe ndiye utakayeshinda.

وَأَلۡقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلۡقَفۡ مَا صَنَعُوٓاْۖ إِنَّمَا صَنَعُواْ كَيۡدُ سَٰحِرٖۖ وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّاحِرُ حَيۡثُ أَتَىٰ﴿٦٩

69Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyoviunda. Hakika walivyounda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo.

فَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سُجَّدٗا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ هَٰرُونَ وَمُوسَىٰ﴿٧٠

70Basi wachawi hao wakaangushwa chini wakasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa!

قَالَ ءَامَنتُمۡ لَهُۥ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِي عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحۡرَۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمۡ فِي جُذُوعِ ٱلنَّخۡلِ وَلَتَعۡلَمُنَّ أَيُّنَآ أَشَدُّ عَذَابٗا وَأَبۡقَىٰ﴿٧١

71(Firauni) akasema: Oh! Mmemuamini kabla ya mimi kuwapa ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi huu. Basi kwa yakini nitawakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Na lazima nitawatundika misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi ndiye mkali zaidi wa kuadhibu na kuiendeleza zaidi adhabu yake.

قَالُواْ لَن نُّؤۡثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلَّذِي فَطَرَنَاۖ فَٱقۡضِ مَآ أَنتَ قَاضٍۖ إِنَّمَا تَقۡضِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَآ﴿٧٢

72Wakasema: Hatutakupendelea wewe kuliko ishara waziwazi zilizotujia, na kuliko yule aliyetuumba. Basi hukumu utavyohukumu; kwani wewe hakika unahukumu tu haya ya maisha ya duniani.

إِنَّآ ءَامَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغۡفِرَ لَنَا خَطَٰيَٰنَا وَمَآ أَكۡرَهۡتَنَا عَلَيۡهِ مِنَ ٱلسِّحۡرِۗ وَٱللَّهُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ﴿٧٣

73Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi uliotulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi (katika kuadhibu).

إِنَّهُۥ مَن يَأۡتِ رَبَّهُۥ مُجۡرِمٗا فَإِنَّ لَهُۥ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ﴿٧٤

74Hakika atakayemjia Mola wake Mlezi naye ni mhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.

وَمَن يَأۡتِهِۦ مُؤۡمِنٗا قَدۡ عَمِلَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلدَّرَجَٰتُ ٱلۡعُلَىٰ﴿٧٥

75Na anayemjia Yeye naye ni Muumini na akatenda mema, basi hao watakuwa na daraja za juu.

جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ مَن تَزَكَّىٰ﴿٧٦

76Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ndiyo malipo ya mwenye kujitakasa.

وَلَقَدۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَسۡرِ بِعِبَادِي فَٱضۡرِبۡ لَهُمۡ طَرِيقٗا فِي ٱلۡبَحۡرِ يَبَسٗا لَّا تَخَٰفُ دَرَكٗا وَلَا تَخۡشَىٰ﴿٧٧

77Na tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja wangu, na uwapigie njia kavu baharini. Usihofu kukamatwa, wala usiogope.

فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ بِجُنُودِهِۦ فَغَشِيَهُم مِّنَ ٱلۡيَمِّ مَا غَشِيَهُمۡ﴿٧٨

78Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kikawafudikiza humo baharini kilichowafudikiza.

وَأَضَلَّ فِرۡعَوۡنُ قَوۡمَهُۥ وَمَا هَدَىٰ﴿٧٩

79Na Firauni aliwapoteza watu wake wala hakuwaongoa.

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ قَدۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ عَدُوِّكُمۡ وَوَٰعَدۡنَٰكُمۡ جَانِبَ ٱلطُّورِ ٱلۡأَيۡمَنَ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰ﴿٨٠

80Enyi Wana wa Israili! Hakika tuliwaokoa kutokana na adui yenu, na tukawaahidi upande wa kulia wa mlima na tukawateremshia Manna na Salwa.

كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَلَا تَطۡغَوۡاْ فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبِيۖ وَمَن يَحۡلِلۡ عَلَيۡهِ غَضَبِي فَقَدۡ هَوَىٰ﴿٨١

81Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyowaruzuku, wala msiruke mipaka katika hayo, isije ikawashukia ghadhabu yangu. Na yule inayemshukia ghadhabu yangu basi huyo ameangamia.

وَإِنِّي لَغَفَّارٞ لِّمَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا ثُمَّ ٱهۡتَدَىٰ﴿٨٢

82Na hakika Mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, kisha akaongoka.

۞ وَمَآ أَعۡجَلَكَ عَن قَوۡمِكَ يَٰمُوسَىٰ﴿٨٣

83Na nini kilichokutia haraka ukawaacha watu wako, ewe Musa?

قَالَ هُمۡ أُوْلَآءِ عَلَىٰٓ أَثَرِي وَعَجِلۡتُ إِلَيۡكَ رَبِّ لِتَرۡضَىٰ﴿٨٤

84Akasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuata. Na nimefanya haraka kukujia, Mola wangu Mlezi, ili uridhike.

قَالَ فَإِنَّا قَدۡ فَتَنَّا قَوۡمَكَ مِنۢ بَعۡدِكَ وَأَضَلَّهُمُ ٱلسَّامِرِيُّ﴿٨٥

85(Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.

فَرَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ أَلَمۡ يَعِدۡكُمۡ رَبُّكُمۡ وَعۡدًا حَسَنًاۚ أَفَطَالَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡعَهۡدُ أَمۡ أَرَدتُّمۡ أَن يَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَخۡلَفۡتُم مَّوۡعِدِي﴿٨٦

86Basi Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakuwaahidi ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ghadhabu ya Mola wenu Mlezi iwashukie, ndiyo maana mkavunja miadi yangu?

قَالُواْ مَآ أَخۡلَفۡنَا مَوۡعِدَكَ بِمَلۡكِنَا وَلَٰكِنَّا حُمِّلۡنَآ أَوۡزَارٗا مِّن زِينَةِ ٱلۡقَوۡمِ فَقَذَفۡنَٰهَا فَكَذَٰلِكَ أَلۡقَى ٱلسَّامِرِيُّ﴿٨٧

87Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa hiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyotupa yule Msamaria.

فَأَخۡرَجَ لَهُمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٞ فَقَالُواْ هَٰذَآ إِلَٰهُكُمۡ وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ﴿٨٨

88Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.

أَفَلَا يَرَوۡنَ أَلَّا يَرۡجِعُ إِلَيۡهِمۡ قَوۡلٗا وَلَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا﴿٨٩

89Je, hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala kuwamilikia kudhuru wala kufaa?

وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي﴿٩٠

90Na hakika Harun alikwishawaambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani (Mwingi wa rehema). Basi nifuateni mimi, na tiini amri yangu!

قَالُواْ لَن نَّبۡرَحَ عَلَيۡهِ عَٰكِفِينَ حَتَّىٰ يَرۡجِعَ إِلَيۡنَا مُوسَىٰ﴿٩١

91Wakasema: Hatutaacha kumwabudu mpaka Musa atakaporejea kwetu.

قَالَ يَٰهَٰرُونُ مَا مَنَعَكَ إِذۡ رَأَيۡتَهُمۡ ضَلُّوٓاْ﴿٩٢

92(Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilichokuzuia, ulipowaona wamepotea?

أَلَّا تَتَّبِعَنِۖ أَفَعَصَيۡتَ أَمۡرِي﴿٩٣

93Usinifuate. Je, umeasi amri yangu?

قَالَ يَبۡنَؤُمَّ لَا تَأۡخُذۡ بِلِحۡيَتِي وَلَا بِرَأۡسِيٓۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقۡتَ بَيۡنَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَمۡ تَرۡقُبۡ قَوۡلِي﴿٩٤

94Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usijesema: Umewatenganisha Wana wa Israili, na hukungojea kauli yangu.

قَالَ فَمَا خَطۡبُكَ يَٰسَٰمِرِيُّ﴿٩٥

95(Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini?

قَالَ بَصُرۡتُ بِمَا لَمۡ يَبۡصُرُواْ بِهِۦ فَقَبَضۡتُ قَبۡضَةٗ مِّنۡ أَثَرِ ٱلرَّسُولِ فَنَبَذۡتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتۡ لِي نَفۡسِي﴿٩٦

96Akasema: Niliona wasiyoyaona wao, nikachukua mkamato wa mkono katika athari za unyayo wa Mtume. Kisha nikaitupa. Na hivi ndivyo ilivyonielekeza nafsi yangu.

قَالَ فَٱذۡهَبۡ فَإِنَّ لَكَ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَۖ وَإِنَّ لَكَ مَوۡعِدٗا لَّن تُخۡلَفَهُۥۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ إِلَٰهِكَ ٱلَّذِي ظَلۡتَ عَلَيۡهِ عَاكِفٗاۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُۥ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُۥ فِي ٱلۡيَمِّ نَسۡفًا﴿٩٧

97(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyovunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliyeendelea kumuabudu. Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya sawasawa baharini.

إِنَّمَآ إِلَٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَسِعَ كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمٗا﴿٩٨

98Hakika mungu wenu ni Allah (Mwenyezi Mungu) tu. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Amekienea kila kitu kwa elimu yake.

كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ مَا قَدۡ سَبَقَۚ وَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ مِن لَّدُنَّا ذِكۡرٗا﴿٩٩

99Namna hivi tunakuhadithia katika khabari za yaliyotangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.

مَّنۡ أَعۡرَضَ عَنۡهُ فَإِنَّهُۥ يَحۡمِلُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وِزۡرًا﴿١٠٠

100Atakayeyapa mgongo, basi kwa yakini Siku ya Kiyama atabeba mzigo.

خَٰلِدِينَ فِيهِۖ وَسَآءَ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ حِمۡلٗا﴿١٠١

101Wadumu humo. Na ni mzigo muovu kwao kuubeba Siku ya Kiyama!

يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ وَنَحۡشُرُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَئِذٖ زُرۡقٗا﴿١٠٢

102Siku litakapopulizwa barugumu, na tukawakusanya wahalifu Siku hiyo, hali macho yao ni ya buluu.

يَتَخَٰفَتُونَ بَيۡنَهُمۡ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا عَشۡرٗا﴿١٠٣

103Watanong'onezana wao kwa wao: Hamkukaa ila siku kumi tu.

نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذۡ يَقُولُ أَمۡثَلُهُمۡ طَرِيقَةً إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا يَوۡمٗا﴿١٠٤

104Sisi tunajua zaidi watakayoyasema, atakaposema mbora wao katika mwendo: Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu.

وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡجِبَالِ فَقُلۡ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسۡفٗا﴿١٠٥

105Na wanakuuliza habari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivurugavuruga.

فَيَذَرُهَا قَاعٗا صَفۡصَفٗا﴿١٠٦

106Na ataiacha tambarare, uwanda.

لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجٗا وَلَآ أَمۡتٗا﴿١٠٧

107Hutaona humo mdidimio wowote wala muinuko.

يَوۡمَئِذٖ يَتَّبِعُونَ ٱلدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُۥۖ وَخَشَعَتِ ٱلۡأَصۡوَاتُ لِلرَّحۡمَٰنِ فَلَا تَسۡمَعُ إِلَّا هَمۡسٗا﴿١٠٨

108Siku hiyo watamfuata muitaji huyo bila ya yeyote kumkengeuka. Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani (Mwingi wa rehema). Basi hutasikia ila mnong'ono tu.

يَوۡمَئِذٖ لَّا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَرَضِيَ لَهُۥ قَوۡلٗا﴿١٠٩

109Siku hiyo uombezi hautafaa kitu, ila kwa atakayeruhusiwa na Arrahmani (Mwingi wa rehema) na akaridhia na maneno yake.

يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِۦ عِلۡمٗا﴿١١٠

110Yeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye vilivyo.

۞ وَعَنَتِ ٱلۡوُجُوهُ لِلۡحَيِّ ٱلۡقَيُّومِۖ وَقَدۡ خَابَ مَنۡ حَمَلَ ظُلۡمٗا﴿١١١

111Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai milele, Msimamia yote milele. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhuluma.

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَا يَخَافُ ظُلۡمٗا وَلَا هَضۡمٗا﴿١١٢

112Na anayetenda katika mema, naye ni Muumini, basi hatahofu kudhulumiwa wala kupunjwa.

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا وَصَرَّفۡنَا فِيهِ مِنَ ٱلۡوَعِيدِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ أَوۡ يُحۡدِثُ لَهُمۡ ذِكۡرٗا﴿١١٣

113Na namna hivi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo vitisho ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho.

فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا﴿١١٤

114Basi ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur-ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu.

وَلَقَدۡ عَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ ءَادَمَ مِن قَبۡلُ فَنَسِيَ وَلَمۡ نَجِدۡ لَهُۥ عَزۡمٗا﴿١١٥

115Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukupata kwake azimio kubwa.

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ﴿١١٦

116Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakasujudu, isipokuwa Iblisi, alikataa.

فَقُلۡنَا يَٰٓـَٔادَمُ إِنَّ هَٰذَا عَدُوّٞ لَّكَ وَلِزَوۡجِكَ فَلَا يُخۡرِجَنَّكُمَا مِنَ ٱلۡجَنَّةِ فَتَشۡقَىٰٓ﴿١١٧

117Tukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wa mkeo. Basi asiwatoe katika Bustani hii, mkaingia mashakani.

إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعۡرَىٰ﴿١١٨

118Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi.

وَأَنَّكَ لَا تَظۡمَؤُاْ فِيهَا وَلَا تَضۡحَىٰ﴿١١٩

119Na hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.

فَوَسۡوَسَ إِلَيۡهِ ٱلشَّيۡطَٰنُ قَالَ يَٰٓـَٔادَمُ هَلۡ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ ٱلۡخُلۡدِ وَمُلۡكٖ لَّا يَبۡلَىٰ﴿١٢٠

120Lakini Shetani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe Adam! Nikujulishe mti wa kuishi maisha ya milele na ufalme usiokoma?

فَأَكَلَا مِنۡهَا فَبَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۚ وَعَصَىٰٓ ءَادَمُ رَبَّهُۥ فَغَوَىٰ﴿١٢١

121Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustanini. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia.

ثُمَّ ٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَتَابَ عَلَيۡهِ وَهَدَىٰ﴿١٢٢

122Kisha Mola wake Mlezi akamteua, na akamkubalia toba yake, na akamwongoa.

قَالَ ٱهۡبِطَا مِنۡهَا جَمِيعَۢاۖ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشۡقَىٰ﴿١٢٣

123Akasema: Ondokeni humo nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uongofu kutoka kwangu basi atakayeufuata uongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.

وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ﴿١٢٤

124Na atakayeupa ukumbusho wangu mgongo, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa ni kipofu.

قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِيٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرٗا﴿١٢٥

125Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona vyema?

قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَٰتُنَا فَنَسِيتَهَاۖ وَكَذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ﴿١٢٦

126(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na vivyo hivyo leo utasahauliwa.

وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَنۡ أَسۡرَفَ وَلَمۡ يُؤۡمِنۢ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦۚ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبۡقَىٰٓ﴿١٢٧

127Na hivyo ndivyo tutakavyomlipa kila apitaye kiasi, na asiziamini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi.

أَفَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ﴿١٢٨

128Je, haikuwabainikia ni ngapi katika vizazi tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye akili.

وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامٗا وَأَجَلٞ مُّسَمّٗى﴿١٢٩

129Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi na muda uliowekwa, bila ya shaka ingefika adhabu (duniani).

فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ غُرُوبِهَاۖ وَمِنۡ ءَانَآيِٕ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡ وَأَطۡرَافَ ٱلنَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرۡضَىٰ﴿١٣٠

130Basi yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla ya kuzama kwake, na nyakati za usiku pia umtakase, na nyakati za mwisho za mchana ili upate ya kukuridhisha.

وَلَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ زَهۡرَةَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا لِنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَرِزۡقُ رَبِّكَ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ﴿١٣١

131Wala kamwe usivikodolee macho tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na yenye kudumu zaidi.

وَأۡمُرۡ أَهۡلَكَ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱصۡطَبِرۡ عَلَيۡهَاۖ لَا نَسۡـَٔلُكَ رِزۡقٗاۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكَۗ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلتَّقۡوَىٰ﴿١٣٢

132Na waamrishe ahali zako kuswali, na usubiri juu yake. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa ucha Mungu.

وَقَالُواْ لَوۡلَا يَأۡتِينَا بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّهِۦٓۚ أَوَلَمۡ تَأۡتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ﴿١٣٣

133Na walisema: "Kwa nini hakutuletea muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Je, haukuwajia ushahidi wazi wa yaliyo katika Vitabu vya mwanzo?

وَلَوۡ أَنَّآ أَهۡلَكۡنَٰهُم بِعَذَابٖ مِّن قَبۡلِهِۦ لَقَالُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ مِن قَبۡلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخۡزَىٰ﴿١٣٤

134Na lau kuwa tuliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: Ewe Mola wetu Mlezi! Kama ungetuletea Mtume (ingekuwa bora), tukazifuata ishara zako kabla ya kudhalilika na kuhizika.

قُلۡ كُلّٞ مُّتَرَبِّصٞ فَتَرَبَّصُواْۖ فَسَتَعۡلَمُونَ مَنۡ أَصۡحَٰبُ ٱلصِّرَٰطِ ٱلسَّوِيِّ وَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ﴿١٣٥

135Sema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni! Hivi karibuni mtajua ni akina nani ndio wenye njia sawa na ni nani aliyeongoka.

RELATED SURAHS