Al-Qalam

القلم

The Pen52 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ﴿١

1Nuun. Ninaapa kwa kalamu na yale wayaandikayo.[1]

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ﴿٢

2Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ﴿٣

3Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika.

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ﴿٤

4Na hakika wewe una tabia tukufu.

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ﴿٥

5Karibu utaona, na wao wataona.

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ﴿٦

6Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ﴿٧

7Hakika Mola wako Mlezi ndiye ajuaye zaidi ni nani aliyeipotea njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ﴿٨

8Basi usiwatii wanaokadhibisha.

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ﴿٩

9Walitamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ﴿١٠

10Wala usimtii kila mwingi wa kuapa, anayedharauliwa.

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ﴿١١

11Mwenye kukejeli mno, anayetangatanga akieneza maneno ya kufitini.

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ﴿١٢

12Mwenye kuzuia mno heri, dhalimu, mwingi wa madhambi.

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ﴿١٣

13Mkatili, na juu ya hayo, ni mshari aliyejipachika tu.

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ﴿١٤

14Ati kwa kuwa ana mali na watoto!

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٥

15Anaposomewa Aya zetu, husema: "(Hizi ni) simulizi za uongo za watu wa zamani!"

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ﴿١٦

16Tutamtia alama kwenye pua yake.

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ﴿١٧

17Hakika tuliwajaribu hawa kama tulivyowajaribu wale wenye shamba, walipoapa kwamba lazima watayavuna mazao yake itakapokuwa asubuhi.

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ﴿١٨

18Wala hawakusema: "Mwenyezi Mungu akipenda!"

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ﴿١٩

19Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ﴿٢٠

20Likawa kama usiku wa giza.

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ﴿٢١

21Kisha asubuhi wakaitana.

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ﴿٢٢

22Ya kwamba: "Nendeni mapema kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna."

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ﴿٢٣

23Basi walikwenda huku wananong'onezana.

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ﴿٢٤

24Ya kuwa: "Leo kamwe masikini mmoja asikuingilieni."

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ﴿٢٥

25Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ﴿٢٦

26Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea!

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ﴿٢٧

27Bali tumenyimwa!

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ﴿٢٨

28Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ﴿٢٩

29Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ﴿٣٠

30Basi wakaelekeana kulaumiana wao kwa wao.

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ﴿٣١

31Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa tumeikiuka mipaka!

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ﴿٣٢

32Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ﴿٣٣

33Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangelijua!

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ﴿٣٤

34Hakika wacha Mungu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ﴿٣٥

35Kwani tutawafanya Waislamu kama wahalifu?

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ﴿٣٦

36Mna nini? Mnahukumu vipi?

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ﴿٣٧

37Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ﴿٣٨

38Kuwa mtapata humo mnayoyapenda?

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ﴿٣٩

39Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayojihukumia?

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ﴿٤٠

40Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa haya?

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ﴿٤١

41Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ﴿٤٢

42Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ﴿٤٣

43Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipokuwa wazima.

فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ﴿٤٤

44Basi niache na wanaokadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kutokea mahali wasipopajua.

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ﴿٤٥

45Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ﴿٤٦

46Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ﴿٤٧

47Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ﴿٤٨

48Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, aliponadi naye kazongwa.

لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٞ﴿٤٩

49Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angelitupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.

فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ﴿٥٠

50Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.

وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٞ﴿٥١

51Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ﴿٥٢

52Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

RELATED SURAHS