الهمزة
The Gossipmonger • 9 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Ole wake kila anayewakejeli watu kwa ishara na maneno.
2Aliyekusanya mali na kuihesabu.
3Anadhani ya kuwa mali yake itambakisha milele!
4Hasha! Hakika atavurumishwa katika Hutwama.
5Na ni nini kitakachokujulisha ni nini Hutwama?
6Ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.
7Ambao unapanda nyoyoni.
8Hakika huo utafungwa sawasawa nao wako ndani yake.
9Kwenye nguzo zilizonyooshwa.