Al-Haqqah

الحاقة

The Inevitable52 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡحَآقَّةُ﴿١

1Tukio la haki.

مَا ٱلۡحَآقَّةُ﴿٢

2Nini hilo Tukio la haki?

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ﴿٣

3Na nini kitakachokujulisha nini hilo Tukio la haki?

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ﴿٤

4Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unaoshtusha.

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ﴿٥

5Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.

وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ﴿٦

6Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika.

سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ﴿٧

7Aliowapelekea usiku saba, na michana minane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yaliyo wazi ndani.

فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ﴿٨

8Basi je! Unamwona mmoja wao aliyebaki?

وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ﴿٩

9Na Firauni na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta dhambi kubwa.

فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً﴿١٠

10Akamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu.

إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ﴿١١

11Maji yalipofurika Sisi tulikupandisheni katika safina.

لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ﴿١٢

12Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalosikia liyahifadhi.

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ﴿١٣

13Na litapopulizwa baragumu mpulizo mmoja tu.

وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ﴿١٤

14Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja.

فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ﴿١٥

15Siku hiyo ndio Tukio litatokea.

وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ﴿١٦

16Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.

وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ﴿١٧

17Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.

يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ﴿١٨

18Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.

فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ﴿١٩

19Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ﴿٢٠

20Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ﴿٢١

21Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza.

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ﴿٢٢

22Katika Bustani ya juu.

قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ﴿٢٣

23Matunda yake ya karibu.

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ﴿٢٤

24Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita.

وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ﴿٢٥

25Na ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: "Laiti nisingelipewa kitabu changu!

وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ﴿٢٦

26Wala nisingelijua nini hisabu yangu.

يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ﴿٢٧

27Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa.

مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ﴿٢٨

28Mali yangu hayakunifaa kitu.

هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ﴿٢٩

29Madaraka yangu yamenipotea."

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ﴿٣٠

30(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!

ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ﴿٣١

31Kisha mtupeni Motoni!

ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ﴿٣٢

32Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini!

إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ﴿٣٣

33Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ﴿٣٤

34Wala hahimizi kulisha masikini.

فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ﴿٣٥

35Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu.

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ﴿٣٦

36Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ﴿٣٧

37Chakula hicho hawakili ila wakosefu.

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ﴿٣٨

38Basi ninaapa kwa mnavyoviona.

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ﴿٣٩

39Na msivyoviona.

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ﴿٤٠

40Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye heshima.

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ﴿٤١

41Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini.

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ﴿٤٢

42Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka.

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ﴿٤٣

43Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ﴿٤٤

44Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu.

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ﴿٤٥

45Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia.

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ﴿٤٦

46Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ﴿٤٧

47Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia kumfikia.

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ﴿٤٨

48Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wacha Mungu.

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ﴿٤٩

49Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha.

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ﴿٥٠

50Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanaokataa.

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ﴿٥١

51Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ﴿٥٢

52Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.

RELATED SURAHS