An-Najm

النجم

The Star62 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ﴿١

1Ninaapa kwa nyota inapotua.

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ﴿٢

2Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ﴿٣

3Wala hatamki kwa matamanio.

إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ﴿٤

4Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.

عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ﴿٥

5Amemfundisha aliye Mwingi wa nguvu.

ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ﴿٦

6Mwenye kutua, akatulia.

وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ﴿٧

7Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ﴿٨

8Kisha akakaribia na akateremka.

فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ﴿٩

9Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.

فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ﴿١٠

10Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alichomfunulia.

مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ﴿١١

11Ufahamu wa moyo wake haukukanusha uliyoyaona.

أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ﴿١٢

12Je, mnabishana naye kwa aliyoyaona?

وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ﴿١٣

13Na akamwona mara nyingine.

عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ﴿١٤

14Penye Mkunazi wa mwisho.

عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ﴿١٥

15Karibu yake ndiyo ipo Bustani ya mbinguni inayokaliwa.

إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ﴿١٦

16Kilipoufunika huo Mkunazi hicho kilichoufunika.

مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ﴿١٧

17Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.

لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ﴿١٨

18Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ﴿١٩

19Je, mmemuona Lata na Uzza?

وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ﴿٢٠

20Na Manaat, mwingine wa tatu?

أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ﴿٢١

21Je, nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?

تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ﴿٢٢

22Huo ni mgawanyo wa dhuluma!

إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ﴿٢٣

23Hayo hayakuwa ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.

أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ﴿٢٤

24Ati mtu anakipata kila anachokitamani?

فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ﴿٢٥

25Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye Akhera na dunia.

۞ وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ﴿٢٦

26Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ﴿٢٧

27Hakika wale wasioamini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.

وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا﴿٢٨

28Nao hawana elimu yoyote kwa hayo isipokuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.

فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا﴿٢٩

29Basi mwachilie mbali anayeupa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.

ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ﴿٣٠

30Huo ndio mwisho wao wa elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anayemjua zaidi mwenye kuongoka.

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى﴿٣١

31Ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo mbinguni na vilivyo katika ardhi, ili awalipe wale waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na wale waliotenda mema awalipe mema.

ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ﴿٣٢

32Ambao wanajiweka mbali na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipokuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijione watakatifu. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga akawa mbali na maovu.

أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ﴿٣٣

33Je, umemwona yule aliyegeuka akaenda zake?

وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ﴿٣٤

34Na akapeana kidogo, kisha akajizuia?

أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ﴿٣٥

35Je, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona?

أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ﴿٣٦

36Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?

وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ﴿٣٧

37Na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi?

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ﴿٣٨

38Ya kwamba hakika nafsi iliyobeba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?

وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ﴿٣٩

39Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe?

وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ﴿٤٠

40Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?

ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ﴿٤١

41Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa hayo kwa ukamilifu.

وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ﴿٤٢

42Na kwamba kwa Mola wako Mlezi ndiyo mwisho.

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ﴿٤٣

43Na kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio.

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا﴿٤٤

44Na kwamba Yeye ndiye anayefisha na kuhuisha.

وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ﴿٤٥

45Na kwamba Yeye ndiye aliyeumba jozi, dume na jike.

مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ﴿٤٦

46Kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa.

وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ﴿٤٧

47Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ﴿٤٨

48Na kwamba ni Yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha.

وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ﴿٤٩

49Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.

وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ﴿٥٠

50Na kwamba Yeye ndiye aliyewaangamiza 'Adi wa kwanza.

وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ﴿٥١

51Na Thamudi hakuwabakisha.

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ﴿٥٢

52Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhalimu zaidi, na waovu zaidi.

وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ﴿٥٣

53Na miji iliyopinduliwa, ni Yeye aliyeipindua.

فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ﴿٥٤

54Vikaifunika vilivyofunika.

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ﴿٥٥

55Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayoifanyia shaka?

هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ﴿٥٦

56Hili ni onyo katika maonyo yale yale ya zamani.

أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ﴿٥٧

57Kiyama kimekaribia!

لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ﴿٥٨

58Hapana wa kukifichua isipokuwa Mwenyezi Mungu.

أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ﴿٥٩

59Je, mnayastaajabia maneno haya?

وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ﴿٦٠

60Na mnacheka, wala hamlii?

وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ﴿٦١

61Nanyi mmeghafilika?

فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩﴿٦٢

62Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.

RELATED SURAHS