Adh-Dhariyat

الذاريات

The Scattering Winds60 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا﴿١

1Ninaapa kwa pepo zinazotawanya.

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا﴿٢

2Na zinazobeba mizigo.

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا﴿٣

3Na zinazokwenda kwa wepesi.

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا﴿٤

4Na zinazogawanya kwa amri.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ﴿٥

5Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni ya ukweli.

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ﴿٦

6Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ﴿٧

7Ninaapa kwa mbingu zenye njia.

إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ﴿٨

8Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayohitalifiana.

يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ﴿٩

9Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.

قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ﴿١٠

10Wazushi wameangamizwa.

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ﴿١١

11Ambao wameghafilika katika ujinga.

يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ﴿١٢

12Wanauliza: 'Ni lini hiyo siku ya malipo?'

يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ﴿١٣

13Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni.

ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ﴿١٤

14Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyokuwa mkiyafanyia haraka.

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ﴿١٥

15Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani ya mbinguni na chemchemi.

ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ﴿١٦

16Wanapokea yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.

كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ﴿١٧

17Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.

وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ﴿١٨

18Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.

وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ﴿١٩

19Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba.

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ﴿٢٠

20Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.

وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ﴿٢١

21Na pia katika nafsi zenu - Je, hamwoni?

وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ﴿٢٢

22Na katika mbingu ziko riziki zenu na yale mnayoahidiwa.

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ﴿٢٣

23Basi ninaapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ﴿٢٤

24Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaoheshimiwa?

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ﴿٢٥

25Walipoingia kwake na wakasema: 'Salama!' Na yeye akasema: 'Salama! Nyinyi ni watu nisiowajua.'

فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ﴿٢٦

26Basi akaenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona.

فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ﴿٢٧

27Akawakaribishia, akasema: 'Mbona hamli?'

فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ﴿٢٨

28Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: 'Usiwe na hofu.' Basi wakambashiria kupata kijana mwenye elimu.

فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ﴿٢٩

29Ndipo mkewe akawaelekea kwa sauti ya kelele huku anajipiga usoni kwa mastaajabu, akasema: "Mimi ni kikongwe na tasa!"

قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ﴿٣٠

30Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua.

۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ﴿٣١

31Akasema: 'Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?'

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ﴿٣٢

32Wakasema: 'Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu.

لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ﴿٣٣

33Tuwatupie mawe ya udongo.

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ﴿٣٤

34Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka.'

فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿٣٥

35Kwa hivyo tukawatoa katika hao wale walioamini.

فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ﴿٣٦

36Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!

وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ﴿٣٧

37Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu.

وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ﴿٣٨

38Na katika habari za Musa, tulipomtuma kwa Firauni na hoja wazi.

فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ﴿٣٩

39Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu!'

فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ﴿٤٠

40Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, huku ni wa kulaumiwa.

وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ﴿٤١

41Na katika habari za 'Adi tulipowatumia upepo wa kukata uzazi.

مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ﴿٤٢

42Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichonyambuka.

وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ﴿٤٣

43Na katika habari za Thamudi walipoambiwa: 'Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.'

فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ﴿٤٤

44Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi ukawanyakua moto wa radi nao wanaona.

فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ﴿٤٥

45Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ﴿٤٦

46Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ﴿٤٧

47Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua.

وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ﴿٤٨

48Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!

وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ﴿٤٩

49Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.

فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ﴿٥٠

50Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.

وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ﴿٥١

51Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.

كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ﴿٥٢

52Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu.'

أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ﴿٥٣

53Je, wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٖ﴿٥٤

54Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.

وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ﴿٥٥

55Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.

وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ﴿٥٦

56Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.

مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقٖ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ﴿٥٧

57Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.

إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ﴿٥٨

58Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.

فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ﴿٥٩

59Hakika wale waliodhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasiniharakishe.

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ﴿٦٠

60Basi ole wao wale walioikanusha siku yao waliyoahidiwa.

RELATED SURAHS