Al-Furqan

الفرقان

The Criterion77 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

تَبَارَكَ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡفُرۡقَانَ عَلَىٰ عَبۡدِهِۦ لِيَكُونَ لِلۡعَٰلَمِينَ نَذِيرًا﴿١

1Ametukuka aliyeteremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖ فَقَدَّرَهُۥ تَقۡدِيرٗا﴿٢

2Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.

وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗ لَّا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ وَلَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا وَلَا يَمۡلِكُونَ مَوۡتٗا وَلَا حَيَوٰةٗ وَلَا نُشُورٗا﴿٣

3Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka.

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّآ إِفۡكٌ ٱفۡتَرَىٰهُ وَأَعَانَهُۥ عَلَيۡهِ قَوۡمٌ ءَاخَرُونَۖ فَقَدۡ جَآءُو ظُلۡمٗا وَزُورٗا﴿٤

4Na wamesema waliokufuru: "Haya si chochote ila ni uzushi aliouzua, na wamemsaidia kwa haya watu wengine!" Hakika hawa wamekuja na dhuluma na uongo.

وَقَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٱكۡتَتَبَهَا فَهِيَ تُمۡلَىٰ عَلَيۡهِ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلٗا﴿٥

5Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyoviandikisha, anavyosomewa asubuhi na jioni.

قُلۡ أَنزَلَهُ ٱلَّذِي يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا﴿٦

6Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

وَقَالُواْ مَالِ هَٰذَا ٱلرَّسُولِ يَأۡكُلُ ٱلطَّعَامَ وَيَمۡشِي فِي ٱلۡأَسۡوَاقِ لَوۡلَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مَلَكٞ فَيَكُونَ مَعَهُۥ نَذِيرًا﴿٧

7Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye?

أَوۡ يُلۡقَىٰٓ إِلَيۡهِ كَنزٌ أَوۡ تَكُونُ لَهُۥ جَنَّةٞ يَأۡكُلُ مِنۡهَاۚ وَقَالَ ٱلظَّٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلٗا مَّسۡحُورًا﴿٨

8Au akaangushiwa hazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema madhalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliyerogwa.

ٱنظُرۡ كَيۡفَ ضَرَبُواْ لَكَ ٱلۡأَمۡثَٰلَ فَضَلُّواْ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ سَبِيلٗا﴿٩

9Tazama jinsi wanavyokupigia mifano. Basi wamepotea, wala hawataiweza Njia.

تَبَارَكَ ٱلَّذِيٓ إِن شَآءَ جَعَلَ لَكَ خَيۡرٗا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَيَجۡعَل لَّكَ قُصُورَۢا﴿١٠

10Ametukuka ambaye akitaka atakujalia yaliyo bora kuliko hayo, nayo ni mabustani yapitayo mito kati yake, na atakujaalia majumba ya fahari.

بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلسَّاعَةِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِمَن كَذَّبَ بِٱلسَّاعَةِ سَعِيرًا﴿١١

11Bali wanaikanusha Saa (ya Kiyama). Na Sisi tumemuandalia Moto mkali kabisa huyo mwenye kuikanusha Saa.

إِذَا رَأَتۡهُم مِّن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ سَمِعُواْ لَهَا تَغَيُّظٗا وَزَفِيرٗا﴿١٢

12Ule Moto ukiwaona tangu mahali mbali, wao watasikia hasira yake na mngurumo wake.

وَإِذَآ أُلۡقُواْ مِنۡهَا مَكَانٗا ضَيِّقٗا مُّقَرَّنِينَ دَعَوۡاْ هُنَالِكَ ثُبُورٗا﴿١٣

13Na watakapotupwa humo mahali penye dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.

لَّا تَدۡعُواْ ٱلۡيَوۡمَ ثُبُورٗا وَٰحِدٗا وَٱدۡعُواْ ثُبُورٗا كَثِيرٗا﴿١٤

14Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!

قُلۡ أَذَٰلِكَ خَيۡرٌ أَمۡ جَنَّةُ ٱلۡخُلۡدِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۚ كَانَتۡ لَهُمۡ جَزَآءٗ وَمَصِيرٗا﴿١٥

15Sema: Je, haya ni bora au Bustani ya milele, ambayo wameahidiwa wacha Mungu, iwe kwao malipo na marejeo?

لَّهُمۡ فِيهَا مَا يَشَآءُونَ خَٰلِدِينَۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ وَعۡدٗا مَّسۡـُٔولٗا﴿١٦

16Watayapata humo wayatakayo daima dawamu. Hii ni ahadi juu ya Mola wako Mlezi, inayoombwa.

وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَقُولُ ءَأَنتُمۡ أَضۡلَلۡتُمۡ عِبَادِي هَٰٓؤُلَآءِ أَمۡ هُمۡ ضَلُّواْ ٱلسَّبِيلَ﴿١٧

17Na siku atakapowakusanya wao na hao wanaowaabudu, na akasema: Je, ni nyinyi mliowapoteza waja wangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia?

قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ مَا كَانَ يَنۢبَغِي لَنَآ أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ وَلَٰكِن مَّتَّعۡتَهُمۡ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ نَسُواْ ٱلذِّكۡرَ وَكَانُواْ قَوۡمَۢا بُورٗا﴿١٨

18Watasema: Subhanaka! (Umetakasika na upungufu!) Haikutupasia sisi kuchukulia walinzi badala yako, lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hata wakasahau kukumbuka, na wakawa watu walioangamia.

فَقَدۡ كَذَّبُوكُم بِمَا تَقُولُونَ فَمَا تَسۡتَطِيعُونَ صَرۡفٗا وَلَا نَصۡرٗاۚ وَمَن يَظۡلِم مِّنكُمۡ نُذِقۡهُ عَذَابٗا كَبِيرٗا﴿١٩

19Basi waliwakanusheni kwa mliyoyasema. Kwa hivyo hamwezi kujiondolea wala kujisaidia. Na atakayedhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa.

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا قَبۡلَكَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّآ إِنَّهُمۡ لَيَأۡكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَيَمۡشُونَ فِي ٱلۡأَسۡوَاقِۗ وَجَعَلۡنَا بَعۡضَكُمۡ لِبَعۡضٖ فِتۡنَةً أَتَصۡبِرُونَۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرٗا﴿٢٠

20Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakienda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio kwa wengine. Je, mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona.

۞ وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ نَرَىٰ رَبَّنَاۗ لَقَدِ ٱسۡتَكۡبَرُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ وَعَتَوۡ عُتُوّٗا كَبِيرٗا﴿٢١

21Na walisema wale wasiotarajia kukutana nasi, "Mbona sisi hatukuteremshiwa Malaika au tumwone nasi Mola wetu Mlezi?" Hakika, hawa wamejiona bora nafsi zao; na wamepanda kichwa, vikubwa mno!

يَوۡمَ يَرَوۡنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ لَا بُشۡرَىٰ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُجۡرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا﴿٢٢

22Siku watakapowaona Malaika, hakutakuwa na furaha yoyote siku hiyo kwa wahalifu. Na watasema, "Mwenyezi Mungu apishe mbali!"

وَقَدِمۡنَآ إِلَىٰ مَا عَمِلُواْ مِنۡ عَمَلٖ فَجَعَلۡنَٰهُ هَبَآءٗ مَّنثُورًا﴿٢٣

23Na tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo na tuyafanye kama mavumbi yaliyotawanywa.

أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ يَوۡمَئِذٍ خَيۡرٞ مُّسۡتَقَرّٗا وَأَحۡسَنُ مَقِيلٗا﴿٢٤

24Watu wa Bustanini siku hiyo watakuwa katika makazi bora na mahali penye starehe nzuri.

وَيَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلسَّمَآءُ بِٱلۡغَمَٰمِ وَنُزِّلَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ تَنزِيلًا﴿٢٥

25Na siku zitakapopasuka mbingu zifunguke kwa mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi.

ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّ لِلرَّحۡمَٰنِۚ وَكَانَ يَوۡمًا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ عَسِيرٗا﴿٢٦

26Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman (Mwingi wa rehema), na itakuwa siku ngumu kwa makafiri.

وَيَوۡمَ يَعَضُّ ٱلظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيۡهِ يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي ٱتَّخَذۡتُ مَعَ ٱلرَّسُولِ سَبِيلٗا﴿٢٧

27Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume!

يَٰوَيۡلَتَىٰ لَيۡتَنِي لَمۡ أَتَّخِذۡ فُلَانًا خَلِيلٗا﴿٢٨

28Ewe ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani!

لَّقَدۡ أَضَلَّنِي عَنِ ٱلذِّكۡرِ بَعۡدَ إِذۡ جَآءَنِيۗ وَكَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لِلۡإِنسَٰنِ خَذُولٗا﴿٢٩

29Hakika alinipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shetani ni haini mkubwa kwa mwanadamu.

وَقَالَ ٱلرَّسُولُ يَٰرَبِّ إِنَّ قَوۡمِي ٱتَّخَذُواْ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ مَهۡجُورٗا﴿٣٠

30Na Mtume alikuwa akisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika kaumu yangu wameifanya hii Qur-ani kuwa ni kihame.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا مِّنَ ٱلۡمُجۡرِمِينَۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيٗا وَنَصِيرٗا﴿٣١

31Na vivyo hivyo tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلۡقُرۡءَانُ جُمۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِۦ فُؤَادَكَۖ وَرَتَّلۡنَٰهُ تَرۡتِيلٗا﴿٣٢

32Na wakasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur-ani yote mara moja tu? Hayo ni hivyo ili tuuimarishe kwayo (ufahamu wa) moyo wako, na ndiyo tumeisoma kwa mafungu.

وَلَا يَأۡتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَأَحۡسَنَ تَفۡسِيرًا﴿٣٣

33Wala hawatakuletea mfano wowote, isipokuwa na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora zaidi.

ٱلَّذِينَ يُحۡشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُوْلَٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ سَبِيلٗا﴿٣٤

34Wale ambao watakusanywa kwa nyuso zao hadi katika Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya mno, nao ndio wenye kuipotea zaidi njia.

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَٰرُونَ وَزِيرٗا﴿٣٥

35Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamuweka pamoja naye kakaye, Harun, kuwa msaidizi.

فَقُلۡنَا ٱذۡهَبَآ إِلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَدَمَّرۡنَٰهُمۡ تَدۡمِيرٗا﴿٣٦

36Tukawaambia: "Nendeni kwa kaumu waliokanusha Ishara zetu." Basi tukawateketeza kabisa.

وَقَوۡمَ نُوحٖ لَّمَّا كَذَّبُواْ ٱلرُّسُلَ أَغۡرَقۡنَٰهُمۡ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ لِلنَّاسِ ءَايَةٗۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِلظَّٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمٗا﴿٣٧

37Na kaumu ya Nuhu, walipowakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia madhalimu adhabu chungu.

وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَأَصۡحَٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونَۢا بَيۡنَ ذَٰلِكَ كَثِيرٗا﴿٣٨

38Na (tuliwaangamiza) kina 'Adi na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyokuwa kati yao.

وَكُلّٗا ضَرَبۡنَا لَهُ ٱلۡأَمۡثَٰلَۖ وَكُلّٗا تَبَّرۡنَا تَتۡبِيرٗا﴿٣٩

39Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa.

وَلَقَدۡ أَتَوۡاْ عَلَى ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِيٓ أُمۡطِرَتۡ مَطَرَ ٱلسَّوۡءِۚ أَفَلَمۡ يَكُونُواْ يَرَوۡنَهَاۚ بَلۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ نُشُورٗا﴿٤٠

40Na kwa yakini wao walikwisha ujia mji ulioteremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.

وَإِذَا رَأَوۡكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي بَعَثَ ٱللَّهُ رَسُولًا﴿٤١

41Na wanapokuona, hawakuchukulii isipokuwa ni mzaha tu, na (wanasema): Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu alimtuma kuwa Mtume?

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنۡ ءَالِهَتِنَا لَوۡلَآ أَن صَبَرۡنَا عَلَيۡهَاۚ وَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ حِينَ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ مَنۡ أَضَلُّ سَبِيلًا﴿٤٢

42Kwa hakika alikuwa karibu zaidi kutupoteza tuiache miungu yetu, lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia.

أَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيۡهِ وَكِيلًا﴿٤٣

43Je, umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?

أَمۡ تَحۡسَبُ أَنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَسۡمَعُونَ أَوۡ يَعۡقِلُونَۚ إِنۡ هُمۡ إِلَّا كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّ سَبِيلًا﴿٤٤

44Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao sio isipokuwa ni kama wanyama tu, bali wao wamepotea zaidi njia.

أَلَمۡ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيۡفَ مَدَّ ٱلظِّلَّ وَلَوۡ شَآءَ لَجَعَلَهُۥ سَاكِنٗا ثُمَّ جَعَلۡنَا ٱلشَّمۡسَ عَلَيۡهِ دَلِيلٗا﴿٤٥

45Je, huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyokitandaza kivuli. Na angelitaka, angelikifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.

ثُمَّ قَبَضۡنَٰهُ إِلَيۡنَا قَبۡضٗا يَسِيرٗا﴿٤٦

46Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا وَٱلنَّوۡمَ سُبَاتٗا وَجَعَلَ ٱلنَّهَارَ نُشُورٗا﴿٤٧

47Naye ndiye aliyewafanyia usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akawafanyia mchana ni kufufuka.

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۚ وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ طَهُورٗا﴿٤٨

48Naye ndiye anayezituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.

لِّنُحۡـِۧيَ بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗا وَنُسۡقِيَهُۥ مِمَّا خَلَقۡنَآ أَنۡعَٰمٗا وَأَنَاسِيَّ كَثِيرٗا﴿٤٩

49Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyokufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tuliowaumba.

وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَٰهُ بَيۡنَهُمۡ لِيَذَّكَّرُواْ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا﴿٥٠

50Na kwa yakini tumeibadilibadili kati yao wapate kukumbuka. Lakini wengi wa watu wanakataa isipokuwa kukufuru tu.

وَلَوۡ شِئۡنَا لَبَعَثۡنَا فِي كُلِّ قَرۡيَةٖ نَّذِيرٗا﴿٥١

51Na tungelitaka, tungelituma katika kila mji Mwonyaji.

فَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَجَٰهِدۡهُم بِهِۦ جِهَادٗا كَبِيرٗا﴿٥٢

52Basi usiwatii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa.

۞ وَهُوَ ٱلَّذِي مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَٰذَا عَذۡبٞ فُرَاتٞ وَهَٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٞ وَجَعَلَ بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٗا وَحِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا﴿٥٣

53Naye ndiye aliyezipeleka bahari mbili, hii ni tamu mno, na hii ni ya chumvi chungu. Na akaweka baina yake kinga na kizuizi kizuiacho.

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ مِنَ ٱلۡمَآءِ بَشَرٗا فَجَعَلَهُۥ نَسَبٗا وَصِهۡرٗاۗ وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرٗا﴿٥٤

54Naye ndiye aliyemuumba mwanadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza mno.

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُهُمۡ وَلَا يَضُرُّهُمۡۗ وَكَانَ ٱلۡكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِۦ ظَهِيرٗا﴿٥٥

55Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyowafaa wala yasiyowadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi.

وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا﴿٥٦

56Nasi hatukukutuma isipokuwa uwe Mbashiri na Mwonyaji.

قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍ إِلَّا مَن شَآءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا﴿٥٧

57Sema: Sikuwaomba ujira wowote juu yake; isipokuwa atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi.

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡحَيِّ ٱلَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِهِۦۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا﴿٥٨

58Na mtegemee aliye Hai, ambaye hafi. Na umtakase kwa sifa zake. Naye anatosha kuwa ndiye Mwenye habari zote za dhambi za waja wake.

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرٗا﴿٥٩

59Ambaye aliziumba mbingu na ardhi, na vilivyo kati yake kwa siku sita. Kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Mwingi wa rehema (Arrahman)! Uliza habari zake kwa amjuaye.[1]

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسۡجُدُواْۤ لِلرَّحۡمَٰنِ قَالُواْ وَمَا ٱلرَّحۡمَٰنُ أَنَسۡجُدُ لِمَا تَأۡمُرُنَا وَزَادَهُمۡ نُفُورٗا۩﴿٦٠

60Na wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!) Wao husema: Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema)? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu? Na huwazidishia kujitenga mbali.

تَبَارَكَ ٱلَّذِي جَعَلَ فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَٰجٗا وَقَمَرٗا مُّنِيرٗا﴿٦١

61Ni Mwenye baraka nyingi yule aliyezijalia nyota mbinguni, na akajalia humo taa na mwezi unaong'ara.

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ خِلۡفَةٗ لِّمَنۡ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوۡ أَرَادَ شُكُورٗا﴿٦٢

62Naye ndiye aliyefanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya yule anayetaka kukumbuka, au anayetaka kushukuru.

وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنٗا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمٗا﴿٦٣

63Na waja wa Arrahman (Mwingi wa rehema) ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza, hujibu: Salama!

وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدٗا وَقِيَٰمٗا﴿٦٤

64Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱصۡرِفۡ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا﴿٦٥

65Na wale wanaosema: "Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi.

إِنَّهَا سَآءَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا﴿٦٦

66Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya."

وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَنفَقُواْ لَمۡ يُسۡرِفُواْ وَلَمۡ يَقۡتُرُواْ وَكَانَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ قَوَامٗا﴿٦٧

67Na wale ambao wanapotoa matumizi, hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubahili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.

وَٱلَّذِينَ لَا يَدۡعُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ وَلَا يَقۡتُلُونَ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَا يَزۡنُونَۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ يَلۡقَ أَثَامٗا﴿٦٨

68Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini. Na atakayefanya hayo, atapata madhara.

يُضَٰعَفۡ لَهُ ٱلۡعَذَابُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَيَخۡلُدۡ فِيهِۦ مُهَانًا﴿٦٩

69Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheshwa.

إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلٗا صَٰلِحٗا فَأُوْلَٰٓئِكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمۡ حَسَنَٰتٖۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا﴿٧٠

70Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda matendo mema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَإِنَّهُۥ يَتُوبُ إِلَى ٱللَّهِ مَتَابٗا﴿٧١

71Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.

وَٱلَّذِينَ لَا يَشۡهَدُونَ ٱلزُّورَ وَإِذَا مَرُّواْ بِٱللَّغۡوِ مَرُّواْ كِرَامٗا﴿٧٢

72Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa heshima yao.

وَٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَمۡ يَخِرُّواْ عَلَيۡهَا صُمّٗا وَعُمۡيَانٗا﴿٧٣

73Na wale ambao wanapokumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu.

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبۡ لَنَا مِنۡ أَزۡوَٰجِنَا وَذُرِّيَّٰتِنَا قُرَّةَ أَعۡيُنٖ وَٱجۡعَلۡنَا لِلۡمُتَّقِينَ إِمَامًا﴿٧٤

74Na wale wanaosema: "Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wana wetu yaburudishayo macho, na utujalie tuwe waongozi kwa wacha Mungu."

أُوْلَٰٓئِكَ يُجۡزَوۡنَ ٱلۡغُرۡفَةَ بِمَا صَبَرُواْ وَيُلَقَّوۡنَ فِيهَا تَحِيَّةٗ وَسَلَٰمًا﴿٧٥

75Hao ndio watakaolipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo maamkizi na salama.

خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ حَسُنَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا﴿٧٦

76Wadumu humo, kituo na makao mazuri kabisa.

قُلۡ مَا يَعۡبَؤُاْ بِكُمۡ رَبِّي لَوۡلَا دُعَآؤُكُمۡۖ فَقَدۡ كَذَّبۡتُمۡ فَسَوۡفَ يَكُونُ لِزَامَۢا﴿٧٧

77Sema: Mola wangu Mlezi asingewajali lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe.

RELATED SURAHS