الفلق
The Daybreak • 5 ayahs • Meccan
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko.
2Kutokana na uovu wa alivyoviumba.
3Na kutokana na uovu wa giza la usiku liingiapo.
4Na kutokana na uovu wa wanaopuliza mafundoni.
5Na kutokana na uovu wa mwenye husuda anapohusudu.