Al-Mursalat

المرسلات

Those Sent Forth50 ayahsMeccan

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا﴿١

1Ninaapa kwa zinazotumwa kwa upole!

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا﴿٢

2Na zinazovuma kwa kasi!

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا﴿٣

3Na zikaeneza maeneo yote!

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا﴿٤

4Na zinazofarikisha zikatawanya!

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا﴿٥

5Na zinazopeleka mawaidha!

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا﴿٦

6Kuwa udhuru au kuonya.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ﴿٧

7Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa!

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ﴿٨

8Wakati nyota zitakapofutwa.

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ﴿٩

9Na mbingu zitakapopasuliwa.

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ﴿١٠

10Na milima itakapopeperushwa.

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ﴿١١

11Na Mitume watakapowekewa wakati wao.

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ﴿١٢

12Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ﴿١٣

13Kwa Siku ya kupambanua!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ﴿١٤

14Na nini kitakachokujuulisha siku ya kupambanua ni nini?

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿١٥

15Ole wao, siku hiyo hao wanaokanusha!

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ﴿١٦

16Kwani hatukuwaangamiza waliotangulia?

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ﴿١٧

17Kisha tukawafuatilizia waliofuatia?

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ﴿١٨

18Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿١٩

19Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ﴿٢٠

20Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?

فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ﴿٢١

21Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?

إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ﴿٢٢

22Mpaka muda maalumu?

فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ﴿٢٣

23Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٢٤

24Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا﴿٢٥

25Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya.

أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا﴿٢٦

26Walio hai na maiti?

وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا﴿٢٧

27Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٢٨

28Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ﴿٢٩

29Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha!

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ﴿٣٠

30Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!

لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ﴿٣١

31Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.

إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ﴿٣٢

32Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!

كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ﴿٣٣

33Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٣٤

34Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ﴿٣٥

35Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu.

وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ﴿٣٦

36Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٣٧

37Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!

هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ﴿٣٨

38Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia.

فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ﴿٣٩

39Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٤٠

40Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ﴿٤١

41Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchemi.

وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ﴿٤٢

42Na matunda wanayoyapenda.

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ﴿٤٣

43Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ﴿٤٤

44Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٤٥

45Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ﴿٤٦

46Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٤٧

47Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ﴿٤٨

48Na wakiambiwa: "Inameni!" Hawainami.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ﴿٤٩

49Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!

فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ﴿٥٠

50Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?

RELATED SURAHS